Marekani yaweka marufuku ya visa kwa wahujumu uchaguzi wa 2023 nchini Nigeria

"Watu hawa wamehusika katika vitisho kwa wapiga kura kupitia vitisho na unyanyasaji wa kimwili, uchakachuaji wa matokeo ya kura, na shughuli nyingine."

Muhtasari

• "Vitendo hivi ni mahususi kwa watu fulani na havielekezwi kwa watu wa Nigeria au Serikali ya Nigeria kwa ujumla,”

Marekani yaweka marufuku kwa wahujumu wa uchaguzi wa Nigeria 2023.
Marekani yaweka marufuku kwa wahujumu wa uchaguzi wa Nigeria 2023.
Image: Twitter//Antony Blinken

Marekani imeweka vikwazo vya visa kwa wanasiasa na watu ambao walihusika katika kuhujumu uchaguzi uliomalizika hivi punde wa 2023 nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Anthony Blinken, katika taarifa yake siku ya Jumatatu, Marekani ilisema imejitolea kuunga mkono matarajio ya Nigeria kuimarisha mchakato wa kidemokrasia na utawala wa sheria.

Blinken, hata hivyo, hakutaja watu ambao watakuwa waathiriwa wa marufuku ya visa.

“Leo, ninatangaza kwamba tumechukua hatua za kuweka vikwazo vya visa kwa watu mahususi nchini Nigeria kwa kuhujumu mchakato wa kidemokrasia wakati wa mzunguko wa uchaguzi wa 2023 wa Nigeria. Vitendo hivi ni mahususi kwa watu fulani na havielekezwi kwa watu wa Nigeria au Serikali ya Nigeria kwa ujumla,” sehemu ya taarifa hiyo ilisoma.

Katika tweet Jumatatu, Blinken alisema, "Tunasalia kujitolea kuunga mkono matarajio ya Nigeria ya kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria."

Chini ya Kifungu cha 212(a)(3)C) cha Sheria ya Uhamiaji na Uraia, watu hawa watawekewa vikwazo vya visa kwenda Marekani chini ya sera inayohusu wale wanaoaminika kuwajibika, au kushiriki katika kuhujumu demokrasia.

Watu hawa wamehusika katika vitisho kwa wapiga kura kupitia vitisho na unyanyasaji wa kimwili, uchakachuaji wa matokeo ya kura, na shughuli nyingine zinazodhoofisha mchakato wa kidemokrasia wa Nigeria, Blinken alisema.