Ndoa za watu wa jinsia moja zilizofanyika nje ya nchi kutambuliwa Namibia

Bado haijabainika wazi uamuzi huu unamaanisha nini kwa sheria za muda mrefu zinapinga uhusiano wa jinsia moja.

Muhtasari
  • Uamuzi huo wa Mahakama ya Juu ya Namibia unafuatia kampeni za wanaharakati wa haki na wanandoa ambao walikuwa wameadhibiwa na sheria zilizopo.

Wakati ndoa za watu wa jinsia moja zikisalia kuwa haramu nchini Namibia, wanandoa wanaofunga ndoa nje ya nchi sasa watatambuliwa nchini humo.

Uamuzi huo wa Mahakama ya Juu ya Namibia unafuatia kampeni za wanaharakati wa haki na wanandoa ambao walikuwa wameadhibiwa na sheria zilizopo.

Chama cha Namibia Equal Rights Movement kilipokea taarifa hiyo kwa kutuma ujumbe kwenye Twitter: "Upendo Unashinda! Asante kwa familia ya Digashu na Sieller-Lilles. Nguvu zenu katika mapambano haya, zimebadilisha taifa hili kwa vizazi vijavyo vya wapenzi wa jinsia moja wa Namibia. #WeBelong."

Kama gazeti la The Namibian linavyoeleza "hukumu ya mahakama inawapa wenzi wasiokuwa Namibia katika ndoa za jinsia moja haki sawa za ukaazi nchini Namibia ambazo zinatolewa kwa wanandoa katika ndoa za jinsia tofauti".

Bado haijabainika wazi uamuzi huu unamaanisha nini kwa sheria za muda mrefu zinapinga uhusiano wa jinsia moja.

KWINGINEKO NI KUWA;

Wizi wa vito vya Dresden: Wanaume watano wapatikana na hatia ya wizi wa 2019

Wanaume watano wamepatikana na hatia ya wizi wa vito katika mji wa Dresden nchini Ujerumani.

Wezi hao waliiba vito vya thamani vya euro milioni 98 kutoka kwa jumba la makumbusho la jiji hilo mnamo 2019.

Polisi walipata vito vingi, ikiwa ni pamoja na upanga wa almasi, lakini inahofiwa hazina iliyobakia insipatikane tena.

Wanaume hao, wote wanachama wa mtandao wa uhalifu, wanakabiliwa na kifungo cha miaka minne hadi sita.

Huu ulikuwa ni wizi uliopangwa kwa uangalifu. Genge hilo, lililokuwa likiishi Berlin, lilitembelea eneo hilo mara kadhaa na kutayarisha mahali pao pa kuingia mapema, kwa kutumia mashine ya kukatia maji ili kuona kupitia sehemu za dirisha la ulinzi kabla ya kuzirudisha mahali pake.