Urusi na Ukraine: Mji wa Kyiv waamkia mashambulizi makali kutoka kwa Urusi

Jumbe za serikali zilionya watu kujiepusha na madirisha

Muhtasari

•      Jumbe za serikali zilionya watu kujiepusha na madirisha huku vifusi vya makombora yaliyozuiwa vikianguka kutoka angani.

Mshambuliai ya Urusi Kyiv
Mshambuliai ya Urusi Kyiv
Image: Reuters

Kuna ripoti za idadi kubwa ya milipuko katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, na ving'ora vya mashambulizi ya anga vimekuwa vikilia.

Katika video kwenye mitandao ya kijamii, mifumo ya ulinzi wa anga inaweza kuonekana ikirusha makombora yanayoshukiwa kuwa ya Kirusi.

Jumbe za serikali zilionya watu kujiepusha na madirisha huku vifusi vya makombora yaliyozuiwa vikianguka kutoka angani.

Meya wa jiji Vitali Klitschko alisema baadhi ya vifusi vya roketi vimeanguka katika wilaya za kati, ikiwa ni pamoja na bustani ya wanyama ya jiji.

Kuna ripoti za majeruhi.

Shambulio hilo tata, ambalo lilitumia ndege zisizo na rubani na makombora, lilielezewa kuwa "la kipekee katika msongamano wake" na afisa mmoja wa Kyiv.

Serhiy Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji mkuu wa Ukraine, alielezea shambulio hilo kuwa na "idadi ya juu zaidi ya makombora ya mashambulizi katika kipindi kifupi zaidi cha muda".

"Kulingana na taarifa za awali, idadi kubwa ya malengo ya adui katika anga ya Kyiv yaligunduliwa na kuharibiwa," aliongeza.