Polisi wazingira nyumba ya Ousmane Sonko wa Senegal

Baadhi ya makabiliano mabaya zaidi yalikuwa katika mji wa kusini wa Ziguinchor, ambapo Sonko ndiye meya.

Muhtasari
  • Bw. Sonko hakuwa mahakani siku ya Alhamisi wakati hukumu ya kifungo cha miaka miwili gerezani ilipotolewa dhidi yake kwa tabia mbaya.
Image: BBC

Polisi katika mji mkuu wa Senegal Dakar, wamezingira makazi ya kiongozi mkuu wa upinzani, Ousmane Sonko, baada ya ghasia kuzuka kufuatia hukumu ya kifungo jela iliyotolewa dhidi yake.

Bw. Sonko hakuwa mahakani siku ya Alhamisi wakati hukumu ya kifungo cha miaka miwili gerezani ilipotolewa dhidi yake kwa tabia mbaya.

Lakini waziri wa haki alisema atafungwa wakati wowote.

Karibu watu tisa waliuawa katika miji ya Dakar na Ziguinchor kusini mwa nchi makabiliano yalipozuka kati ya wafuasi wa Sonko na polisi.

Serikali ya Senegal imefungia baadhi ya mitandao ya kijamii ikisisitiza kuwahatua hiyo itasaidia kudumisha utulivu.

Takriban watu tisa wameuawa wakati wa makabiliano kati ya polisi wa kutuliza ghasia na waandamanaji nchini Senegal baada ya kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko, kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Walioathirika walitangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Antoine Diome katika mkutano na waandishi wa habari usiku wa manane baada ya siku ya ghasia kote nchini.

Bw Diome alisema kuwa mitandao ya kijamii kama vile Facebook na WhatsApp imefungwa.

Baadhi ya makabiliano mabaya zaidi yalikuwa katika mji wa kusini wa Ziguinchor, ambapo Sonko ndiye meya.

Kifungo cha jela - ambacho kilitolewa akiwa hayupo - kinaweza kumzuia kiongozi huyo wa upinzani kugombea uchaguzi wa urais mwaka ujao.

Alipatikana na hatia ya tabia mbaya, lakini akaondolewa ubakaji.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa alipatikana kuwa alitenda usherati kwa mtu mwenye umri wa chini ya miaka 21.

Mashtaka hayo yalitokana na madai yaliyotolewa na mtaalamu wa masaji.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa upinzani amekana kufanya kosa lolote.

Serikali ya Senegal inasema itachukua hatua zote zinazohitajika kulinda watu na mali kufuatia machafuko hayo mabaya.