Watoto waliopotea kwa siku 40 baada ya ajali ya ndege wapatikana hai msituni

Watoto hao walikuwa na umri wa miaka 13, 9, 4, na 1 mtawalia na wamekuwa wakizurura msituni wakiwa peke yao tangia Mei tarehe 1.

Muhtasari

• “Leo tumeshuhudia siku ya kimiujiza,” rais wan chi hiyo Petro Gustavo aliwambia wanahabari.

Watoto waliopotea katika ajali ya ndege kwa siku 40 wapatikana wakiwa hai.
Watoto waliopotea katika ajali ya ndege kwa siku 40 wapatikana wakiwa hai.
Image: Twitter//Gustavo Petra

Watoto wane waliotoweka kwa takribani siku 40 tangu ajali ya ndege katika msitu mmoja nchini Kolombia wamepatikana wakiwa hai.

Kulingana na jarida la AFP, watoto hao wanne walinusurika kwenye ajali hiyo ila hawakupatikana na taarifa za kipindi hicho ziliwatangaza kuwa waliangamia kwenye mkasa wa ndege ndogo iliyoanguka kwenye msitu wa Amazon huko Kolombia.

Kulingana na taarifa, watoto hao walivutwa kutoka kwa mabaki hayo na kuwekwa kwenye ndege ya kijeshi tayari kukimbizwa hospitalini.

Maafisa wa polisi waliambia jarida hilo kwamba walichokiona ni kama muujiza kwani hakuna aliyeuwa anadhania kwamba mtu angepatikana akiwa hai, siku 40 baada ya ajali.

“Leo tumeshuhudia siku ya kimiujiza,” rais wan chi hiyo Petro Gustavo aliwambia wanahabari.

Alisema kuwa watoto hao walikuwa wamekonda na kuishiwa nguvu huku akitoa nafasi kwa madaktari kufanya juhudi zao ili kunyoosha afya zao.

“Furaha kwa nchi nzima! Watoto 4 waliopotea siku 40 zilizopita katika msitu wa Colombia walionekana hai,” rais Gustavo Petro aliandika kwenye Twitter yake.

Watoto hao walikuwa na umri wa miaka 13, 9, 4, na 1 mtawalia na wamekuwa wakizurura msituni wakiwa peke yao tangia Mei tarehe 1 wakati ambapo ndege waliyokuwa ndani ilipata ajali.