Mapigano mapya yazuka Sudan baada ya mapatano ya kusitisha mapigano ya 24 kumalizika

Mapigano makali yamezuka tena kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Rapid Support Forces baada ya kumalizika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku moja.

Muhtasari

• Pia, wakaazi katika maeneo ya mashariki mwa mto Nile walithibitisha kuwa mapigano makali yalizuka kati ya jeshi na vikosi vya Rapid Support Forces ambapo silaha nzito zilitumika pia.

• Wakaazi katika maeneo ya mashariki mwa mto Nile walithibitisha kuwa mapigano makali yalizuka kati ya jeshi na vikosi vya Rapid Support Forces ambapo silaha nzito zilitumika pia.

Mapigano makali yamezuka tena kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Rapid Support Forces,alfajiri ya Jumapili, katika maeneo kadhaa kwenye mji mkuu, Khartoum, baada ya kumalizika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku moja.

Walioshuhudia walisema kwamba mapigano yalianza tena saa kumi na mbili asubuhi kaskazini mwa Omdurman, moja ya miji mitatu jirani, pamoja na Khartoum na Bahri, ambayo kwa pamoja yanaunda mji mkuu karibu na makutano ya Mto Nile, muda mfupi baada ya mwisho wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Waliongeza, katika mahojiano na BBC, kwamba mapigano makali yalitokea kati ya pande hizo mbili karibu na Daraja la Halfaya huko Bahri, kuashiria kuwa silaha nzito zilitumika katika mapigano hayo.

Pia, wakaazi katika maeneo ya mashariki mwa mto Nile walithibitisha kuwa mapigano makali yalizuka kati ya jeshi na vikosi vya Rapid Support Forces ambapo silaha nzito zilitumika pia.

Nchi hiyo ilishuhudia hali ya utulivu adimu siku ya Jumamosi, baada ya pande mbili za mzozo huo kujitolea kwa mapatano kwa saa ishirini na nne, ambapo silaha zilinyamaza baada ya wiki 8 za mapigano makali.

Usitishaji vita wa hivi karibuni ulikuwa mzuri zaidi kuliko ule wa awali, kwani utulivu uliruhusu watu kuweka akiba ya bidhaa za msingi, lakini gharama zao kubwa na ugumu wa kuzipata ulifanya iwe jambo gumu kwa wananchi.