logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tetetemko la ardhi lauwa watu 623 nchini Morocco

Tetemeko hilo lilitokea saa 23:11 siku ya Ijumaa. Kulikuwa na mshtuko wa 4.9 dakika 19 baadaye.

image
na Davis Ojiambo

Habari09 September 2023 - 08:40

Muhtasari


  • • Tetemeko hilo lilitokea saa 23:11 siku ya Ijumaa. Kulikuwa na mshtuko wa 4.9 dakika 19 baadaye.
  • • Watu walikufa huko Marrakesh na maeneo kadhaa ya kusini, wizara ilisema. Wengi wa waathiriwa wanaaminika kuwa katika maeneo ya mbali.
Mtetemeko wa ardhi Morocco.

Usiku wa kuamkia Jumamosi, hali ya taharuki ilitanda katika mji wa kihistoria wa Marrakesh mchini Morocco baada ya tetemeko baya Zaidi la ardhi kutokea na kuwaua angalau watu 632, runinga ya BBC News imeripoti Jumamosi asubuhi.

Kitovu hicho kilikuwa katika Milima ya Juu ya Atlas, 71km (maili 44) kusini-magharibi mwa Marrakesh, kwa kina cha kilomita 18.5, Utafiti wa Jiolojia wa Marekani ulisema.

Tetemeko hilo lilitokea saa 23:11 siku ya Ijumaa. Kulikuwa na mshtuko wa 4.9 dakika 19 baadaye.

Watu walikufa huko Marrakesh na maeneo kadhaa ya kusini, wizara ilisema. Wengi wa waathiriwa wanaaminika kuwa katika maeneo ya mbali.

Wizara ya mambo ya ndani ilinukuliwa na BBC kwamba tetemeko la ardhi liliua watu katika majimbo na manispaa ya al-Haous, Marrakesh, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant, na kuongeza kuwa watu wasiopungua 329 wamejeruhiwa.

Klipu za video ambazo hazijathibitishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha majengo yaliyoharibiwa, majengo mengine yakitikiswa na mitaa iliyojaa vifusi. Watu wanaonekana wakikimbia kwa hofu.

Baadhi ya majengo katika mji huo mkongwe yameporomoka, mkazi mmoja aliambia shirika la habari la Reuters. Klipu kadhaa kwenye X zinaonyesha majengo yakianguka, lakini BBC haijatambua ni wapi yalikuwa.

Wenyeji wanasemekana kuamua kusalia nje ya nyumba zao iwapo jiji hilo litatikiswa na mitetemeko mikubwa ya baadaye.

Mwanamume mwingine katika jiji hilo la kihistoria alielezea kuhisi "tetemeko kali" na kuona "majengo yakisonga".

"Watu wote walikuwa na mshtuko na hofu. Watoto walikuwa wakilia na wazazi walikuwa wamefadhaika," Abdelhak El Amrani aliambia shirika la AFP.

 

Alisema umeme na laini za simu zilikatika kwa dakika 10.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved