logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu 10,000 wamepotea baada ya mafuriko makubwa nchini Libya - IFRC

Mahali palipoathirika zaidi ni bandari ya Derna, ambayo sehemu kubwa iko chini ya maji.

image
na Davis Ojiambo

Habari13 September 2023 - 05:14

Muhtasari


  • • Takriban watu 10,000 wanakisiwa kupotea kufuatia mafuriko makubwa nchini Libya kulingana na shirika la  IFRC.

Takriban watu 10,000 wanakisiwa kupotea kufuatia mafuriko makubwa nchini Libya kulingana na afisa kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC).

"Tunaweza kuthibitisha kutoka kwa vyanzo vyetu huru vya habari kwamba idadi ya watu waliopotea inafikia 10,000 hadi sasa," alisema Tamer Ramadan, mkuu wa ujumbe wa IFRC nchini Libya.

Mafuriko na maporomoko ya udongo yanayosababishwa na mvua kubwa yameharibu barabara na nyumba nyingi.

Mahali palipoathirika zaidi ni bandari ya Derna, ambayo sehemu kubwa iko chini ya maji baada ya mabwawa mawili na madaraja manne kuporomoka.

"Idadi ya vifo ni kubwa na huenda ikafikia maelfu," aliongeza Bw Ramadan.

IFRC inaweza hivi karibuni kuwasilisha ombi la ufadhili wa dharura kusaidia wahanga wa mafuriko nchini Libya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved