•Rafiki yake, mwenye umri wa miaka 63, aliyeshambuliwa kwenye miguu yote miwili na fahali mmoja alitibiwa na sasa yuko katika hali nzuri hospitalini.
•Vifo na majeraha wakati wa matamasha ya mbio za mafahali nchini Uhispania sio kawaida.
Mwanamume mmoja amefariki na rafiki yake kujeruhiwa wakati wa tamasha la mbio za mafahali mashariki mwa Uhispania, mamlaka inasema.
Mwanamume huyo, mwenye umri wa miaka 61, alipigwa ubavuni mwake na ng’ombe wakati wa hafla hiyo katika mji wa Pobla de Farnals katika eneo la Valencia siku ya Jumamosi. Alifanyiwa upasuaji wa dharura lakini alifariki Jumapili.
Rafiki yake, mwenye umri wa miaka 63, aliyeshambuliwa kwenye miguu yote miwili na fahali mmoja alitibiwa na sasa yuko katika hali nzuri hospitalini.
Vifo na majeraha wakati wa matamasha ya mbio za mafahali nchini Uhispania sio kawaida.
Kuna mamia ya matukio kama haya - ambapo mafahali hutolewa kwenye barabara za jiji huku watu wakikimbia mbele yao - kote Uhispania kila mwaka.
Mashirika ya kutetea haki za wanyama kwa muda mrefu yamekuwa yakilalamikia hatari hiyo kwa umma pamoja na wanyama.
Lakini matukio haya ya kila mwaka yameendelea kuwa maarufu.
Msimu wa mbio za mafahali hutoa huboresha sana uchumi wa Valencia.
Utafiti wa 2019 uligundua kuwa mbio hizi zilisaidia kubuni ajira 3,000 na kuingiza pato la euro milioni 300. Karibu matukio kama haya 10,000 hufanyika kila mwaka.