Wanajeshi 5 wa Marekani wafariki katika ajali ya ndege ya mafunzo mashariki mwa Mediterania

Ndege hiyo ilipata hitilafu ilipokuwa ikijaza mafuta ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya kawaida.

Muhtasari

•Rais Joe Biden alitoa rambirambi kwa waathiriwa, akisema wahudumu waliweka " maisha yao kwa ajili ya nchi yetu kila siku".

Image: BBC

Wanajeshi watano wa Marekani wamefariki katika ajali ya helikopta mashariki mwa Mediterania, jeshi la Marekani limesema.

Inasema ndege hiyo ilipata hitilafu ilipokuwa ikijaza mafuta ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya kawaida.

Marekani imeongeza operesheni zake katika eneo hilo tangu kuzuka kwa mzozo kati ya Israel na Hamas.

Rais Joe Biden alitoa pongezi kwa waathiriwa, akisema wahudumu waliweka " maisha yao kwa ajili ya nchi yetu kila siku".

"Tunasali kwa ajili ya familia za wapiganaji wetu wote waliofariki leo na kila siku," aliongeza.

Taarifa hiyo ya jeshi haikubainisha ni wapi ndege hiyo ilikuwa ikiruka au ni wapi iilikotokea ajali hiyo.

Lakini Marekani imehamisha ndege mbili za kubeba mizigo, pamoja na jeti, hadi mashariki mwa Mediterania katika kipindi cha mwezi uliopita.

Hatua hiyo inaonyesha wasiwasi wa Marekani kwamba mzozo kati ya Israeli na Hamas unaweza kuenea katika maeneo mengine ya eneo hilo.

Marekani ina nia hasa ya kuzuia vuguvugu lenye nguvu la Hezbollah la Lebanon kujiunga na mzozo huo.

Hezbollah Inaungwa mkono na Iran, ambayo pia inafadhili na kuipatia silaha Hamas.