logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ubakaji wa watoto na mauaji ya kikabila yafichuliwa nchini Sudan - UN

Inapendekeza maelfu ya watu wameuawa katika mashambulizi ya kikabila katika eneo la Darfur

image

Habari23 February 2024 - 15:09

Muhtasari


  • Ripoti hiyo inahusu miezi minane baada ya mzozo huo kuzuka mwezi wa Aprili mwaka jana na ina ushahidi kutoka kwa mamia ya watu.

Ripoti ya Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeweka wazi ukiukaji wa kutisha unaofanywa na pande zote mbili katika vita nchini Sudan.

Ripoti hiyo inahusu miezi minane baada ya mzozo huo kuzuka mwezi wa Aprili mwaka jana na ina ushahidi kutoka kwa mamia ya watu.

Inapendekeza maelfu ya watu wameuawa katika mashambulizi ya kikabila katika eneo la Darfur na inajumuisha madai ya watoto kubakwa.

Picha za satelaiti zinaonyesha kuenea kwa matumizi ya vilipuzi vizito kwenye maeneo yenye watu wengi, na kuua idadi kubwa ya raia.

Ripoti hiyo inajiri baada ya kanda za video kuibuka wiki hii za wanafunzi wakikatwa vichwa na wanaume waliovalia sare ambao baadaye waliviweka vichwa vilivyokatwa kwenye vijiti barabarani.

Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na mazungumzo jumuishi kuelekea serikali ya kiraia nchini Sudan.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved