Msanii wa filamu akamatwa kwa tuhuma za mauaji ya shabiki wake

Mashitaka wanayokabiliwa nayo ni mauaji, utekaji nyara, uharibifu wa Ushahidi na kushiriki katika kupanga njama ya kihalifu.

Muhtasari
  • Darshan ni miongoni mwa watu 17 waliokamatwa na polisi kwa kushukiwa kuhusika katika mauaji ya Renukaswamy- kijana mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa shabiki mkubwa wa muigizaji huyo

Darshan Thoogudeepa, ni muigizaji mwenye umaarufu mkubwa ambaye fiolamu zake huandaliwa kwa lugha ya kannada inayozungumzwa katika jimbo la Karnataka lililopo kusini mwa India, amekuwa akizuiliwa na polisi nchini humo kwa siku kumi zilizopita kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji yaliyofanyika kama inavyoigizwa kwenye filamu ambazo ni mhusika mkuu.

Darshan ni miongoni mwa watu 17 waliokamatwa na polisi kwa kushukiwa kuhusika katika mauaji ya Renukaswamy- kijana mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa shabiki mkubwa wa muigizaji huyo. – walikamatwa baada ya mwili wake kupatikana katika mtaro.

Mapema wiki hii , Kamishena mkuu wa polisi katika mji wa Bengaluru alisema kwamba Renukaswamy aliuawa katika hali ya ukatili na kueleza mauaji hayo kama kisa kibaya cha jinai.

Polisi nchini India wanaamini kwaman muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 47 alikuwa na hasira dhidi ya Renukaswamyambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya kutengeneza dawa, kwa sababu anadaiwa kutuma ujumbe zenye maneno makali ya kingono kupitia mitandao ya kijamii kwa Pavithra Gowda, muigizaji wa kike ambaye ametambulishwa katika vyombo vya Habari nchini India kama mpenzi wake Darshan.

Gowda ni miongoni mwa waliokamatwa.

Mashitaka wanayokabiliwa nayo ni mauaji, utekaji nyara, uharibifu wa Ushahidi na kushiriki katika kupanga njama ya kihalifu.

Darshan anaziliwa na polisi na hajazungumzia madai dhidi yake lakini wakili wake Ranganath Reddy ameiambia BBC kwamba wanapokutana, muigizaji huyo akina mashataka dhidi yake.

‘'Haya ni madai tu kwa sasa,'’ alisema. ‘ Polisi hawana ushahidi wa moja kwa moja kumhusu Darshan. Ni kesi ambayo haina Ushahidi wa moja kwa moja.’ Bwana Reddy pia amesema kwamba madai ya kuwa Pavitha alikuwa mke wa Darshan ni uongo mtupu.