Mtoto ahofiwa kuliwa na mamba nchini Australia

Polisi wanasema timu ya wataalamu wa utafutaji na uokoaji imetumwa baada ya "ripoti za awali kusema mtoto huyo alishambuliwa na mamba".

Muhtasari
  • Eneo hilo ina makadirio ya mamba 100,000 wa maji ya chumvi, zaidi ya mahali pengine popote duniani, lakini mashambulizi si ya kawaida.

Msako mkali unaendelea kaskazini mwa Australia kumtafuta mtoto anayehofiwa kuchukuliwa na mamba.

Mtoto mwenye umri wa miaka 12 alionekana mara ya mwisho jioni ya Jumanne, akiogelea karibu na mji wa mbali wa Nganmarriyanga umbali wa takribani saa 7 kwa gari kuelekea kusini magharibi mwa Darwin.

Polisi wanasema timu ya wataalamu wa utafutaji na uokoaji imetumwa baada ya "ripoti za awali kusema mtoto huyo alishambuliwa na mamba".

Eneo hilo ina makadirio ya mamba 100,000 wa maji ya chumvi, zaidi ya mahali pengine popote duniani, lakini mashambulizi si ya kawaida.

Wanajamii huko Nganmarriyanga, hapo awali ilijulikana kama Palumpa na makazi ya watu 364 pekee na polisi wa eneo hilo walianza kumtafuta mtoto huyo mara baada ya kutoweka mwendo wa 17:30 saa za ndani (08:00 GMT).

Sasa wameunganishwa na maafisa wa ziada na timu ya utaftaji na uokoaji wa kitaalamu ambao wanatafuta nchi kavu na majini.

Utafutaji wa angani unaweza pia kuanza, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.