logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanachama zaidi waandamizi wa chama cha democratic wamtaka Biden kutowania urais

Rais pia ataangaziwa katika siku zijazo huku akiandaa mkutano wa kilele wa viongozi

image

Habari08 July 2024 - 14:02

Muhtasari


  • Maoni mbalimbali juu ya kugombea kwa Bw Biden yanatarajiwa kujitokeza zaidi siku ya Jumatatu baada ya wabunge kurejea Capitol Hill.

Wabunge wengine kadhaa waandamizi wa chama cha Rais Joe Biden cha Democratic wamejiunga na wito wa kumtaka akabidhi ugombea wake katika uchaguzi wa Novemba kwa mgombea mwingine, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

Wakati wa mazungumzo na Kiongozi wa walio Wachache Bungeni Hakeem Jeffries, wabunge wanne walizungumza wazi kumtaka Bwana Biden ajiondoe, kulingana na vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News.

Wanne hao waliungwa mkono na wengine ambao walionyesha wasiwasi wao juu ya uwezo wa Bw Biden kuendelea kushikilia ofisi hiyo baada ya utendaji mbaya wa mjadala wa hivi majuzi, lakini hawakumuomba rais kujiondoa, CBS iliongeza.

Bw Biden ameapa kuendelea kuwa kinyang’anyironi, na amedumisha uungwaji mkono wa Wanademokrasia wengine ambao wanasisitiza kuwa yeye ndiye mtu atakayemshinda Donald Trump katika kura ya Novemba.

Maoni mbalimbali juu ya kugombea kwa Bw Biden yanatarajiwa kujitokeza zaidi siku ya Jumatatu baada ya wabunge kurejea Capitol Hill.

Rais pia ataangaziwa katika siku zijazo huku akiandaa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Nato huko Washington.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved