Benki kuu, vyombo vya habari na mashirika ya ndege kwa sasa yanakabiliwa na hitilafu kubwa za IT.
Safari za ndege zimesimamishwa katika uwanja wa ndege wa Sydney, United Airlines imeacha kupaa angani , na jukwaa soko la hisa la London Stock Exchange linakabiliwa na hitilafu .
Hitilafu ya IT : Nini kinatokea?
- Ripoti za kukatika kwa IT zinakuja kutoka kote ulimwenguni
- Mashirika ya ndege, mashirika ya utangazaji na benki zimeathirika - ikiwa ni pamoja na Sky News nchini Uingereza, ambayo haipo hewani
- Viwanja vingi vya ndege nchini Uingereza na duniani kote vinaripoti kuchelewa, na baadhi ya safari za ndege zimesitishwa
- Nchini Marekani, mashirika makubwa ya ndege yakiwemo United na Delta yamesimamisha safari za ndege
- Nchini Australia, viwanja vya ndege, maduka na mawasiliano vimeathirika, Mratibu wa Kitaifa wa Usalama wa Mtandao wa Australia akielezea kama "kukatika kwa huduma za kiufundi kwa kiasi kikubwa"
- Kampuni za reli nchini Uingereza zinaripoti ucheleweshaji
- Microsoft inasema inaendelea kukabiliana na "athari zinazoendelea" za kukatika kwa huduma za kiteknolojia