Idadi ya watu waliouawa katika maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia imeongezeka na kufikia takriban 146, maafisa wa eneo hilo wamesema.
Matukio mawili yanakisiwa kutokea Jumapili jioni na Jumatatu asubuhi, baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo la mbali la milima la ukanda wa Gofa.
Mamlaka ya eneo hilo ilisema kuwa utafutaji wa manusura ulikuwa "unaendelea" lakini "idadi ya vifo bado inaweza kuongezeka".
Picha zilionyesha mamia ya watu wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la tukio na wengine wakichimba chini ya vifusi kutafuta watu walionasa.
Kwa nyuma, sehemu ya kilima inaweza kuonekana ikiwa imeporomoka kiasi na sehemu kubwa ya ardhi yenye udongo mwekundu.
Meskir Mitku, msimamizi mkuu wa eneo la Gofa, alisema wanawake, watoto na maafisa wa polisi walikuwa miongoni mwa waliopoteza maisha.
"Kulikuwa na mvua kubwa jana [Jumapili] usiku na baadhi ya watu walifariki kutokana na maporomoko ya ardhi," msemaji wa serikali wa wilaya ya Gofa Kassahun Abayneh alisema.
Gofa ni sehemu ya jimbo linalojulikana kama Kusini mwa Ethiopia, lililoko karibu kilomita 320 (maili 199) kusini-magharibi mwa mji mkuu, Addis Ababa.
Taarifa ya idara ya mawasiliano ya eneo la Gofa ilisema kuwa idadi ya waliofariki imepita 146, na inaweza kuongezeka zaidi, AFP inaripoti.
Kusini mwa Ethiopia ni miongoni mwa maeneo ya nchi hiyo ambayo yamekumbwa na mvua kubwa na mafuriko katika miezi ya hivi karibuni, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (Ocha).
Lakini matukio ya maporomoko ya ardhi na mafuriko yamekuwa yakitokea siku za nyuma. Mnamo mwezi Mei 2016, takriban watu 50 waliuawa katika mafuriko na maporomoko ya ardhi kufuatia mvua kubwa kusini mwa nchi.