Thomas Matthew Crooks, 20, ambaye alimpiga risasi Donald Trump katika mkutano wa kampeni huko Pennsylvania, alitafuta mtandao wa maelezo zaidi kuhusu mauaji ya Rais wa Marekani John F. Kennedy siku kadhaa kabla ya shambulio hilo, Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray alitoa ushahidi katika kikao cha bunge.
Alisema uchanganuzi wa mawakala wa tarakilishi wa Crooks ulionyesha kwamba alipendezwa, pamoja na mambo mengine, jinsi Lee Harvey Oswald, ambaye alimpiga risasi Kennedy huko Dallas mnamo Novemba 1963, alivyokuwa mbali kutoka kwa rais.
"Mwezi Julai 6, aliingia katika mtandao wa Google na kutakakujua 'Oswald alikuwa umbali gani kutoka kwa Kennedy?'" Wray aliwaambia wajumbe wa Kamati ya Bunge.
"Utafutaji huo bila shaka una umuhimu mkubwa katika suala la hali yake ya kiakili."
"Inaonekana alijiandikisha kwa mkutano wa hadhara huko Butler siku hiyo hiyo," mkuu wa FBI alisema.
Wray pia alisema Crooks alitumia ndege isiyo na rubani kuchunguza eneo la mkutano takriban saa mbili kabla ya Trump kupanda jukwaani.Ndege hiyo isiyo na rubani ilikuwa angani kwa dakika 11.
Ndege hiyo isiyo na rubani na rimoti yake zilipatikana kwenye gari la mshambuliaji huyo pamoja na vifaa viwili vya vilipuzi.
Bomu lingine lilipatikana katika nyumba ya Crooks, Wray aliongeza.
Mkurugenzi wa FBI alisema bado hakuna ushahidi kwamba Crooks alikuwa na washirika na kwamba alionekana kuwa alitenda uhalifu huo peke yake.