• Naibu spika wa bunge alitangaza mapumziko baada ya mapigano ya ngumi.
• Kufuatia mapumziko ya zaidi ya saa tatu, kikao hicho kiliitishwa tena, safari hii kikiongozwa na spika wa bunge badala ya naibu wake.
Vita vya ngumi vilizuka katika bunge la Uturuki siku ya Ijumaa wakati mwaasiasa wa mrengo wa upinzani alishambuliwa na wenzake kutoka mrengo wa serikali kwa kile kilichotajwa kuwa ni kutaka mbunge mwenzake aliyeko jela kuachiliwa huru.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mbunge huyo wa upinzani aliyeko jela alifungwa kwa madai ya kuandaa maandamano dhidi ya serikali lakini tangu achaguliwe kama mbunge, hajawahi kubaliwa kuhudhuria vikao vya bunge.
Kanda za video kwenye jukwaa la X zilionyesha wabunge wa chama tawala cha AKP wakikimbilia kumpiga mbunge kwa jina Ahmet Sik kwenye ukumbi wa mikutano na makumi ya wengine wakijiunga na vurugu, baadhi wakijaribu kuwazuia wengine.
Damu zilitapakaa kwenye zulia jeupe la jukwaa la spika wa bunge hilo.
Mbunge huyo anayetuhumiwa kwa kuandaa maandamnao dhidi ya serikali kwa jina Atalay alihukumiwa kifungo cha miaka 18 mwaka wa 2022 baada ya kushtakiwa kwa kujaribu kupindua serikali kwa madai ya kuandaa maandamano ya kitaifa ya Gezi Park mnamo 2013 na mfadhili Osman Kavala, ambaye pia amefungwa, na wengine sita, Reuters waliripoti.
Licha ya kufungwa kwake, Atalay alichaguliwa kuwa mbunge Mei mwaka jana kuwakilisha Chama cha Wafanyakazi cha Uturuki (TIP).
Bunge lilimvua kiti chake, lakini Agosti 1 Mahakama ya Kikatiba ilitangaza kutengwa kwake kuwa batili.
Naibu spika wa bunge alitangaza mapumziko baada ya mapigano ya ngumi.
Kufuatia mapumziko ya zaidi ya saa tatu, kikao hicho kiliitishwa tena, safari hii kikiongozwa na spika wa bunge badala ya naibu wake.
Ugomvi, ingawa ni nadra, hausikiki katika bunge la Uturuki. Mnamo Juni, wabunge wa AKP walizozana na wabunge wanaounga mkono Wakurdi wa Chama cha DEM kuhusu kuzuiliwa na kubadilishwa kwa meya wa Chama cha DEM kusini-mashariki mwa Uturuki kwa madai ya kuhusishwa na wanamgambo.