"Tuchague ukweli, tuchague heshima, tuchague furaha," Winfrey aliuambia umati uliokuwa ukishangilia siku ya Jumatano.
Nguli wa televisheni Oprah Winfrey amejitokeza bila kutarajiwa katika Kongamano la Kitaifa la chama cha Democrats katika mji alikozaliwa wa Chicago, ambapo aliwataka wafuasi wa chama hicho na wapiga kura wasioegemea upande wowote "kuchagua busara badala ya upuuzi".
"Tuchague ukweli, tuchague heshima, tuchague furaha," Winfrey aliuambia umati uliokuwa ukishangilia siku ya Jumatano. "Kwa sababu hiyo ndiyo Marekani bora zaidi."
Winfrey, ambaye ameepuka kujiingiza kwenye kisiasa katika miaka ya hivi majuzi, alionyesha kujionea fahari Makamu wa Rais Kamala Harris na mgombea mwenza wake, gavana wa Minnesota Tim Walz katika usiku wa tatu wa kongamano la siku nne.
Kuwaunga mkono wawili hao kumesaidia kuipa nguvu zaidi chama cha Democtrats - ambacho wiki hii kimeshuhudia kujitokeza kwa watu wengi maarufu kama vile rapper Lil Jon.