Usalama waimarishwa huku mahakama ikitoa uamuzi kuhusu BBI

Muhtasari

• Polisi wanasema wameimarisha ulinzi katika eneo hilo kama tahadhari.

• Kuna masuala saba muhimu ambayo yalitolewa katika rufaa hiyo.

• Rufaa hiyo iliyowasilishwa na mwanasheria mkuu Kihara Kariuki miongoni mwa wengine.

Jaji wa Mahakama ya Juu Philomena Mwilu, Jaji Mkuu Martha Koome, majaji wa Mahakama ya Juu Mohamed Ibrahim na Njoki Ndung'u wakati wa kusikilizwa kwa rufaa ya BBI katika mahakama ya juu Januari 18, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A
Jaji wa Mahakama ya Juu Philomena Mwilu, Jaji Mkuu Martha Koome, majaji wa Mahakama ya Juu Mohamed Ibrahim na Njoki Ndung'u wakati wa kusikilizwa kwa rufaa ya BBI katika mahakama ya juu Januari 18, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A

Usalama umeimarishwa karibu na Mahakama ya Juu ambapo majaji wanatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mchakato wa BBI leo Alhamisi.

Polisi wanasema wameimarisha ulinzi katika eneo hilo kama tahadhari.

Majaji wa mahakama ya juu watatoa uamuzi wao kuhusu rufaa ya BBI iliyowasilishwa na mwanasheria mkuu Kihara Kariuki miongoni mwa wengine.

Kuna masuala saba muhimu ambayo yalitolewa katika rufaa hiyo.

Mchakato wa BBI ulisitishwa baada ya mahakama kuu kuharamisha mchakato huo kwa kile mahakama ilisema ni kutozingatia sheria wakati wa kuandaa msuada wa marebisho ya katiba maarufu BBI.

Msuada huo ulikuwa unapigiwa debe na rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga.

Miongoni mwa masuala mengine msuada huo ulikuwa unapendekeza kuongezwa kwa mgao wa fedha za serikali za kaunti, kuongeza idadi ya wanawake bungeni na kuongeza idadi ya maeneo bunge.