Jamaa ashtakiwa kwa kubaka mwanamke aliyemtumia video chafu

Muhtasari

•Karatasi ya mashtaka ilisema mshtakiwa alimbaka PQ katika mtaa wa la Laini Saba, eneo la Kibera ndani ya Kaunti ya Nairobi.

•Wawili hao walitazama video hiyo pamoja na baadaye wakakubaliana kukaa kidogo kwa nyumba ya mshtakiwa, ambapo inasemekana alitenda kosa hilo.

Benard Ndung'u katika mahakama ya Kibera Jumanne
Benard Ndung'u katika mahakama ya Kibera Jumanne
Image: CLAUSE MASIKA

Mfanyibiashara mmoja anayedaiwa kumbaka mwanamke muda mfupi baada ya kumtumia video ya ngono amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kibera.

Benard Ndungu Ngumbi alishtakiwa Jumanne  mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa Kibera Phillip Mutua.  Mshtakiwa alikanusha mashtaka.

Karatasi ya mashtaka ilisema mshtakiwa alimbaka PQ katika mtaa wa la Laini Saba, eneo la Kibera ndani ya Kaunti ya Nairobi.

Ndung’u alishtakiwa kwa kosa la pili la kufanya kitendo kisichofaa na mtu mzima kinyume na sheria.

Alikanusha mashtaka yote na akaachiliwa kwa bondi ya Sh200,000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Mahakama ilisikia kwamba mlalamishi alituma video ya ponografia kwa simu ya mshtakiwa na baadaye kumtembelea katika eneo lake la kazi.

Ilisemekana kuwa mshtakiwa alikuwa katika kibanda ambapo huwa anauza nguo kando ya Barabara ya Reli katika kaunti ndogo ya Kibera wakati mwanamke huyo alipomtembelea.

Kisha walitazama video hiyo pamoja na baadaye wakakubaliana kukaa kidogo kwa nyumba ya mshtakiwa, ambapo inasemekana alitenda kosa hilo.

Kesi hiyo itatajwa tena Juni 6.