Maagizo ya muda ya mahakama hayatanizuia kutumikia wananchi-Sonko

Muhtasari
  • Mwanasiasa huyo mahiri alisisitiza kuwa sheria iko wazi kabisa, akionyesha kujiamini kuwa atakuwa na kicheko cha mwisho
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko
Image: Facebook// Mike Sonko

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema kuwa ataendelea kuwahudumia watu wa Mombasa.

Katika taarifa ya Jumanne, Sonko anayewania kiti cha ugavana Mombasa alisema hata maagizo mbalimbali ya mahakama ya muda hayatampunguza kasi.

Mwanasiasa huyo mahiri alisisitiza kuwa sheria iko wazi kabisa, akionyesha kujiamini kuwa atakuwa na kicheko cha mwisho.

"Hizi ma interim orders za kuni block hazitatu punguza tusifanyie wanainchi kazi. Sheria iko wazi kabisa, tuone nani atacheka mwisho," Sonko aliandika.

Matamshi ya gavana huyo wa zamani wa Nairobi yanajiri huku kukiwa na maombi mbalimbali ya kutaka azuiwe kuwania wadhifa wa umma kwa sababu alitimuliwa.

Watu binafsi na makundi ya washawishi yamekuwa yakitoa wito kwa taasisi husika kumzuia Sonko na aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu kushikilia afisi yoyote ya umma.

Mnamo Mei 10, mahakama ilizuia Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka(IEBC) kuwaondoa magavana waliotimuliwa Mike Sonko na Ferdinand Waititu kushiriki katika uchaguzi wa Agosti 9.

Pia matamshi yake Sonko yanajiri sku moja baada ya mwanake mmoja kuhamia kortini na kumshataki mwanasiasa huyo kwa kutelekeza mtoto wao.

Huku akijibu madai hayo Sonko alisema hatatoa chcochote.