Maombi ya mauti! mwanamke afa njaa baada ya kufunga kwa kipindi kirefu

Muhtasari

• Maafisa wa polisi wanashuku marehemu alifariki kutokana na njaa baada kipindi kirefu cha kufunga na maombi.

Crime scene
Crime scene

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu mwili wa mwanamke mkongwe uliopatikana maeneo ya Nyayo, Embakasi.

Maafisa wa polisi wanashuku marehemu alifariki kutokana na njaa baada kipindi kirefu cha kufunga na maombi.

Inasemekana alikuwa katika mfungo kwanzia tarehe kumi nane Mei. Familia yake ilisema kuwa walipata mwili wa marehemu kitandani baada ya kuvunja mlango wake uliokuwa umefungwa kwa ndani. 

Kwingineko, mwanamume wa miaka hamsini na moja alianguka na kufariki alipokuwa akifanya mazoezi mitaa ya Koinange, Nairobi. Mashahidi walisema kuwa marehemu alianguka alipokuwa akikimbia kwenye mashine ya ‘treadmill’. Alifikishwa hospitalini akiwa tayari ameaga dunia. 

Huku hayo yakijiri, maafisa wa polisi wamemkamata mwanamke aliyesemekana kumuua mumewe kwa kumdunga kisu kutokana na ugomvi wa kinyumbani mtaani Mathare. Polisi walifika katika eneo la tukio hilo na kuupeleka mwili katika hifadhi ya maiti, mshukiwa anasubiri kufunguliwa mashtaka baada ya uchunguzi kukamilika. 

Aidha, katika maneo ya Tassia jijini Nairobi, mwili wa mwanamume ulipatikana ukining’inia nyumbani mwake. Marehemu alipatikana baada ya kuripotiwa kutoweka.