DPP hana mamlaka ya kuwashtaki washukiwa wa uhalifu-Mahakama

Muhtasari
  • Mrima aliamua kuwa ni ODPP pekee ndiye aliye na mamlaka ya kisheria ya kuendesha kesi
Mahakama
Mahakama

Mahakama ya rufaa imesitisha uamuzi ulioipa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) mamlaka ya kuandaa mashtaka.

Mahakama ya rufaa siku ya Alhamisi ilisitisha utekelezaji wa hukumu ya Jaji Antony Mrima iliyosema kuwa ni ofisi ya DPP ambayo inaweza kuandaa hati za mashtaka.

Katika kesi iliyowasilishwa na Humphrey Kariuki na wenzake saba dhidi ya ODPP, mahakama ya Hakimu Mkuu, Mahakama ya Milimani na DCI, Jaji Mrima alikuwa ameamua kuwa DCI haina mamlaka ya kisheria ya kushtaki kesi.

Kariuki alikuwa amewasilisha ombi la kupinga karatasi ya mashtaka iliyotumiwa kumshtaki akisema iliandaliwa kinyume cha sheria na DCI badala ya ODPP.

Jaji Mrima alikubaliana na wasilisho lao na akazuia mahakama yoyote kuchukua hatua kuhusu suala lolote lililofunguliwa na DCI.

Mrima aliamua kuwa ni ODPP pekee ndiye aliye na mamlaka ya kisheria ya kuendesha kesi.

Lakini Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikata rufaa dhidi ya kesi hiyo akidai Mrima alikosea katika uamuzi wake.