(Video) Mama aliyemuua mwanawe wa asili ya Kenya akishirikiana na baba wa kambo ahukumiwa UK

Mahakama iliambiwa baba kambo alichukia sura ya Logan iliyokaribiana na ya babake wa asili ya Kenya,

Muhtasari

• Mahakama iliambiwa kwamba Cole alichukia sura ya Logan iliyokaribiana na ya babake asili, ambaye ni wa asili ya Kenya, katika kile kinachoenekana kuwa ubaguzi wa rangi unaweza kuwa ulichangia mtazamo wake kwa Logan.

Mvulana mwenye umri wa miaka mitano Logan Mwangi aliuawa na mama yake, babake wa kambo na kijana wa miaka 14 baada ya miezi kadhaa ya unyanyasaji na kufungwa katika "gereza" la chumba chake kidogo cha giza, mahakama imebaini.

Baada ya Logan Mwangi kufariki kutokana na majeraha ambayo huwa yanawakuta watu ambao wamehusika katika ajali ya barabarani au kuanguka kutoka urefu, washukiwa Angharad Williamson mamake, John Cole babake wa kambo na mvulana huyo walijaribu kukwepa haki kwa kuutupa mwili wa mvulana huyo mtoni na kuwapigia simu polisi kuripoti kuwa huenda alikuwa ametekwa nyara.

Mahakama iliambiwa kwamba Cole alichukia sura ya Logan iliyokaribiana na ya babake asili, ambaye ni wa asili ya Kenya, katika kile kinachoenekana kuwa ubaguzi wa rangi unaweza kuwa ulichangia mtazamo wake kwa Logan.

Williamson alipopatikana na hatia, alianguka chini, akipiga kelele: "Hapana, hapana, hapana." Alipokuwa akiongozwa kutoka kortini, Williamson alisukumana na maafisa wa mahakama na kumzomea Cole: "Wewe muuaji mwongo."

Nje ya mahakama, babake Logan, Ben Mwangi, alisema: “Logan alikuwa mvulana maridadi na wa kupendeza zaidi. Ulimwengu ni mahali baridi na giza zaidi bila tabasamu yake ya joto na furaha. Nilimpenda sana na inabidi niishi maisha yangu nikijua kwamba sitawahi kumuona akikua na kuwa mtu mzuri ambaye angekuwa.”