Msichana wa miaka 15 asimulia mahakamani jinsi alivyonajisiwa

Mlalamishi alisema shambulio hilo lilishuhudiwa na mamake ambaye alikuja kumsaidia.

Muhtasari

•Msichana huyo alisema mshtakiwa alimvamia akidai kuwa alikuwa amevaa koti la kijana mwingine.

•Mshtakiwa alikanusha mashtaka dhidi yake na kupewa bondi ya Sh300,00 lakini bado yuko rumande.

Mahakama
Mahakama

Mwanamume mmoja ameshtakiwa kwa kumnajisi mtoto wa umri wa miaka 15 kati ya Agosti hadi Desemba 2019 katika mtaa wa Southlands,eneo la Lang'ata, Nairobi.

Victor Oduor Otieno alikanusha mashtaka na kupewa bondi ya Sh300,00 lakini bado yuko rumande.

Msichana huyo alitoa ushahidi mahakamani kuhusu jinsi mshtakiwa alivyomnajisi mara kadhaa.

Alisema kisa cha kwanza kilitokea alipokuwa akiishi katika nyumba ya mshtakiwa huko Lang'ata.

Mlalamishi aliambia mahakama kuwa siku moja alipokuwa nyumbani kwa dadake Otieno, mshtakiwa alikuja na kumpeleka chumbani kwake na kumnajisi.

Msichana huyo aliambia mahakama kuwa dada ya mshtakiwa hakuwahi kujua kuhusu kisa hicho.

Alisema siku nyingine mshtakiwa alimvamia akidai kuwa alikuwa amevaa koti la kijana mwingine.

"Aliniambia kwa kuwa nilikuwa mpenzi wake na aliona wivu kuniona nikivaa koti hilo," alisema.

Mhasiriwa aliambia mahakama shambulio hilo lilishuhudiwa na mamake ambaye alikuja kumsaidia.

Alisema baadaye alimjulisha mamake kuwa mshtakiwa alikuwa akimnajisi.

"Mama yangu alinipeleka hospitalini baadaye tuliripoti suala hilo kwa polisi," alisema.

Hakimu mkuu mwandamizi wa Kibera Derrick Kuto aliagiza kesi hiyo isikizwe mwezi ujao