Mshtakiwa alimwambia jirani yake alilala na mbwa, mahakama yaambiwa

Jicho lake la kulia lilijeruhiwa vibaya sana. Wamoja alifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya Kibera William Tulei.

Muhtasari
  • Robai Wamoja alikuwa amekiri kosa la kumpiga mwanamke huyo na kumsababishia madhara mwilini alipompiga usoni kwa ndoo
Image: CLAUSE MASIKA

Mahakama ya Kibera ilishtuka siku ya Ijumaa baada ya upande wa mashtaka kusema mwanamke aliyemshambulia jirani yake pia alisema kuwa alikuwa kahaba ambaye alilala na mbwa.

Robai Wamoja alikuwa amekiri kosa la kumpiga mwanamke huyo na kumsababishia madhara mwilini alipompiga usoni kwa ndoo.

Jicho lake la kulia lilijeruhiwa vibaya sana. Wamoja alifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya Kibera William Tulei.

Hati ya mashtaka ilisomeka kuwa alimshambulia mnamo Juni 30 katika eneo la Kangemi Gichagi kaunti ya Nairobi

Upande wa mashtaka ulisoma kwa sauti, "Mshtakiwa alisema mlalamikaji ni kahaba na wakati huo huo akamwambia amelala na mbwa wote ndani ya Kawangware."

Mahakama ilisikia mlalamishi alikuwa ameenda kwenye bomba mbele ya nyumba ya mshtakiwa wakati mshtakiwa alipomtusi.

Alichukua ndoo na kumpiga mwanamke huyo usoni. Mwanamke huyo aliripoti shambulio hilo kwa polisi.

Wamoja alikamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kangemi.

Alikiri alitenda kosa hilo lakini akaomba msamaha, akisema alikuwa mama wa nyumbani kutoka katika malezi duni. Yeye ni mkosaji wa mara ya kwanza. Aliagizwa kulipa faini ya Sh20,000 au kukaa jela miezi sita.

Alipewa siku 14 kukata rufaa.