Mahakama yamtaka marehemu Jacob Juma kurudisha shamba alilonyakua, kulipa fidia 50M

Hakimu aliagiza warithi wa Juma kulipa fidia ya milioni 50 pamoja na kurudisha shamba hilo kwa wamiliki halali.

Muhtasari

• Raia hao wa kigeni katika malalamishi yao walisema kwamba Juma alikuwa na dola kipindi hicho na baada ya kunyakua ardhi yao aliizungushia ua la mawe na kuwafungia nje.

Mfanyibiashara hayati Jacob Juma
Mfanyibiashara hayati Jacob Juma
Image: Twitter//JacobJuma

Mahakama ya mazingira na Ardhi Alhamis imetoa imeagiza mfanyibiashara hayati Jacob Juma kurudisha shamba moja lililoko jijini Nairobi kwa wenyewe katika kile ambacho mahakama hiyo ilitajka kwamba Juma alinyakua ardhi hiyo kinyume na sheria.

Hakimu Loice Koi Komingoi alisema kwamba Juma alihitiliafiana na hatimiliki za shamba hilo kwa kushirikiana na badhi ya maafisa katika afisi zinashoshughulikia Ardhi ambao walimuundia hatimiliki bandia ili kupata umiliki wa shamba hilo lililotajwa kuwa la thamani ya shilingi milioni 500 pesa za benki kuu ya Kenya.

Shamba hilo linatajwa kuwa na wamiliki halali ambao ni raia wa kigeni Ashok Shah na Hitenkumar Raja, na Juma alilinyakua kutoka kwao mwaka 2008.

Akitaja kesi hiyo, hakimu Komingoi alimtaka hayati Jacob Juma kuwalipa wamiliki halali hao wawili kiasi cha shilingi milioni 50 kama fidia ya kuwapoza kwa madhara aliyowasababishia kunyimwa umiliki halali wa shamba lao.

“Juma aliingilia kinyume cha sheria na kunyakua mali hiyo kuanzia 2008, wakati shamba kuu la Loresho, Nairobi, lilipokadiriwa kuwa lenye thamani ya KSh 252 milioni. Nimeridhishwa kuwa walalamishi wamepata hasara kwa kuingiliwa katika mali yao kwa njia isiyo halali na wana haki ya kufidiwa KSh 50 milioni,” hakimu Komingoi aliamuru.

Raia hao wa kigeni katika malalamishi yao walisema kwamba Juma alikuwa na dola kipindi hicho na baada ya kunyakua ardhi yao aliizungushia ua la mawe na kuwafungia nje.

Kutokana na kwamba mshatkiwa hakuwa hai wakati wa uamuzi wa kesi hiyo ambayo imekuwa mahakamani kwa muda mrefu, hakimu Komingoi aliwataka warithi wa Juma kutekeleza uamuzi huo wa kuondoka katika ardhi hiyo na kuirudisha kwa wamiliki halali pamoja na kulipa fidia ya milioni 50.

Mfanyabiashara Jacob Juma aliuawa mwaka 2016 katika barabara ya Ngong jijini Nairobi ambapo alipatikana amepigwa risasi ndani ya gari lake, baada ya kuzozana na watu kadhaa kutokana na ufichuzi wenye utata kuhusu watu fulani nchini alioufanya kwenye ukurasa wake wa Facebook.