Si jukumu letu kuamua mawakili halisi wa IEBC - Mahakama ya upeo

Muhtasari
  • Mahakama ya upeo imesema si jukumu lake kusuluhisha ni wakili gani atakayewakilisha IEBC katika Mahakama ya Juu
Benchi la majaji saba likiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome, naibu CJ Lady Justice Philomena Mwilu, Jaji Mohammed Ibrahim, Jaji Dkt. Smokin Wanjala, Lady Justice Njoki Ndungu, Jaji Isaac Lenaola na Jaji William Ouko wakati wa kongamano la kesi kabla ya kuanza kwa ombi la urais katika Mahakama ya Juu Agosti 30, 2022.
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mahakama ya upeo imesema si jukumu lake kusuluhisha ni wakili gani atakayewakilisha IEBC katika Mahakama ya Juu.

Katika uamuzi wake Jumanne, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu alisema mzozo kati ya makamishna ni wa ndani.

"Mahakama hii haiwezi kushughulikia suala au mzozo wa uwakilishi wa kisheria wa IEBC katika ombi hili," alisema.

"Tumezingatia shauri. Sio shughuli ya mahakama bali ni suala la ndani ambalo lazima lisuluhishwe na IEBC na makamishna. Mahakama hii haitoweza. kuingizwa kwenye mzozo huu."

Mwilu alisema makamishna hao wanne wanaweza kutumia huduma za Paul Muite kama wataona ni muhimu katika shughuli hiyo.