Kindiki aeleza kwa nini Chebukati hakusubiri hadi Jumanne kutangaza mshindi

Kindiki alikuwa akijibu swali la Jaji Isaac Lenaola kuhusu kwa nini Chebukati hakuwasiliana na makamishna hao wanne ili kupata muafaka.

Muhtasari
  • Kindiki alisema haiwezekani kwa sababu ya kutoelewana kwa dakika za mwisho kati ya makamishna hao
WAKILI KITHURE KINDIKI
Image: EZEKIEL AMING'A

Wakili Kithure Kindiki Ijumaa alijibu swali la majaji kuhusu ni kwa nini mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati hakutangaza matokeo siku ya saba.

Chebukati alikuwa na hadi Jumanne, Agosti 16, kutangaza matokeo kwa mujibu wa sheria.

Kindiki alisema haiwezekani kwa sababu ya kutoelewana kwa dakika za mwisho kati ya makamishna hao.

“Matokeo hayakuweza kutangazwa siku iliyofuata kwa sababu kwa mujibu wa hati ya kiapo ya mwenyekiti wa tume, wakati huo haikuwezekana kuwepo kwa maridhiano ya aina yoyote,” alisema.

"Ilikuwa wazi kwamba nia ilikuwa kujaribu kupinga matakwa ya wananchi na hivyo mwenyekiti alipaswa kutangaza matokeo hayo."

Kindiki alikuwa akijibu swali la Jaji Isaac Lenaola kuhusu kwa nini Chebukati hakuwasiliana na makamishna hao wanne ili kupata muafaka.