James Ndichu apatikana na hatia ya kuwapa wateja dawa kinyume cha sheria kwa malengo ya kuwanajisi

Wendy alisema upande wa mashtaka ulithibitisha kesi yake bila shaka dhidi yake.

Muhtasari
  • Katika utetezi wake, Mugo alimtaka hakimu kumwachilia huru kwa kukosa ushahidi
  • Aliteta kuwa hakuwahi kukutana na mwanamke aliyedaiwa kumbaka katika kliniki yake
Daktari James Mugo Ndichu,
Image: DOUGLAS OKIDDY

Daktari James Mugo Ndichu, almaarufu Wairimu, amepatikana na hatia ya kuwapa wagonjwa dawa kinyume cha sheria katika kliniki yake mwaka wa 2015.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Wendy Micheni mnamo Alhamisi aligundua kuwa Mugo, ambaye alishtakiwa kwa makosa 12 alikuwa na hatia ya makosa 10.

Mahakama ilimtia hatiani kwa kuendesha kituo cha matibabu kinyume cha sheria, kuwapa wagonjwa wake dawa kinyume cha sheria miongoni mwa wengine.

Wendy alisema upande wa mashtaka ulithibitisha kesi yake bila shaka dhidi yake.

Hata hivyo, ameachiwa huru kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa wake na kuwaajiri wanafunzi wawili kinyume cha sheria kufanya naye kazi katika zahanati yake kutokana na kukosekana kwa ushahidi.

Katika utetezi wake, Mugo alimtaka hakimu kumwachilia huru kwa kukosa ushahidi.

Aliteta kuwa hakuwahi kukutana na mwanamke aliyedaiwa kumbaka katika kliniki yake.