Mfanyabiashara ashtakiwa kwa kuiba Sh3.1 milioni

Aliomba masharti nafuu ya dhamana na nakala za maelezo ya mashahidi kutoka kwa upande wa mashtaka.

Muhtasari
  • Upande wa mashtaka umepanga mashahidi sita kutoa ushahidi katika kesi hiyo
Mahakama ya Milimani mjini Nairobi
Mahakama ya Milimani mjini Nairobi

Mfanyabiashara mmoja Jumanne alishtakiwa kwa kuiba Sh3.1 milioni kutoka kwa kampuni kwa njia za uwongo.

Nancy Wambui Gachoki alishtakiwa kwa kuiba pesa hizo kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya Almex sevens limited ambazo alikuwa amepokea kwa ajili ya kampuni hiyo au kwa akaunti yake.

Alidaiwa kutenda kosa hilo mnamo Septemba 30, 2022, katika kampuni ya motorship dealers Limited kando ya barabara ya Kiambu.

Wambui anasemekana kuiba pesa hizo kwa kuwa wakala wa kampuni hiyo.

Alikanusha mashtaka mbele ya hakimu mkuu wa Milimani Luka Kimaru.

Aliomba masharti nafuu ya dhamana na nakala za maelezo ya mashahidi kutoka kwa upande wa mashtaka.

Upande wa mashtaka umepanga mashahidi sita kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Hakimu alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh300,000 au bondi ya Sh800,000.