Pasta Ezekiel kusalia korokoroni kwa siku 2 zaidi

Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Shanzu Joe Omido aliagiza kwamba kesi hiyo itatajwa Mei 4.

Muhtasari
  • Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Shanzu Joe Omido aliagiza kwamba kesi hiyo itatajwa Mei 4
  • Mhubiri huyo alikamatwa Aprili 27 na polisi walikuwa wameomba azuiliwe kwa siku 30 kusubiri kukamilika kwa uchunguzi

Mchungaji Ezekiel Odero atalala korokoroni usiku mwingine katika Kituo cha Polisi cha Bandari.

Hii ni baada ya mahakama kuagiza kuwa kesi yake itasikizwa Mei 4.

Mhubiri huyo alikamatwa Aprili 27 na polisi walikuwa wameomba azuiliwe kwa siku 30 kusubiri kukamilika kwa uchunguzi.

Lakini mahakama imeruhusu polisi kumzuilia kwa siku saba.

Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Shanzu Joe Omido aliagiza kwamba kesi hiyo itatajwa Mei 4.

Ijumaa iliyopita, Odero alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Shanzu baada ya kushtakiwa kwa kutenda kosa la mauaji, kusaidia kujiua, utekaji nyara, itikadi kali, mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili wa watoto, ulaghai na utakatishaji fedha.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai aliwasilisha hati ya kiapo akiomba mahakama imnyime Odero masharti ya dhamana kwa sababu uhalifu unaochunguzwa kwa asili, uzito na uzito wake ni tata.

Odero pia anahusishwa na mhubiri mwenye utata kutoka Malindi, Paul Mackenzie, ambaye pia yuko rumande kwa madai ya vifo vya wafuasi wake huko Shakahola huko Magarini, Kilifi.

Kwa sababu ya muda uliowekwa kama matokeo ya muda wa kikatiba wa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa washukiwa, Mahakama ya Shanzu ilitenga Mei 2 kwa ajili ya kutoa uamuzi huo baada ya kusikiliza muhtasari wa mdomo wa pande zote mbili.

Kukamatwa kwa Odero ni kufuatia kile ambacho DCI walitaja kuwa wana tarifa za kijasusi ambazo zinamhusisha na Mackenzie, wakisema kuwa baadhi ya watu ambao walifariki karika kanisa lake walisafirishwa kwa lori kwenda Shakahola kwa shamba la Mackenzie kwa ajili ya maziko.

Hata hivyo, Salasya alimtetea vikali Odero  siku ya Ijumaa na alizitaka idara zote kufanya uchunguzi wao dhidi ya Mackenzie pasi na kumuingiza Odero kwenye sakata hilo.

“Mchungaji Ezekiel anapaswa kuachwa mbali na matatizo yanayoletwa na Mackenzie. Polisi, DCI, mwendesha mashitaka, EACC, mahakama n.k walipata fursa ya kuwalinda wananchi waliopotoshwa kifikira lakini badala yake walinyamaza .Hakuna anayepaswa kumvamia mchungaji Ezekiel, kama amepata kituo, tatizo nini?” aliuliza Salasya.

Alhamisi baada ya Odero kukamatwa, mbunge wa Magarini Harrison Kombe alikuwa mtu wa kwanza kumtetea mwinjilisti huyo akisema kuwa anaamini katika miujiza yake kwani kwa kipindi kimoja aliwahi kufika katika kanisa lake na kusujudu.

“Kuna watu wametoka katika eneo bunge langu na kwenda mpaka kanisa la Ezekiel kwa ajili ya maombi na kurudi wakiwa katika hali salama. Na pia kwa ufahamu, ni kwamba sasa hivi Ezekiel anajenga chuo cha madaktari katika eneo lake,” Kombe alisema.