Jowie aeleza jinsi alivyojipiga risasi kwa ajili ya ujumbe

Mahakama pia ilisikia kuhusu jinsi alivyopata bunduki inayodaiwa kumilikiwa na jirani yake.

Muhtasari
  • Irungu alifikishwa mbele ya Jaji Grace Nzioka katika mahakama ya Milimani huku kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani ikiendelea.

Jowie Irungu, mshukiwa wa mauaji ya Monica Kimani, alifika kortini mnamo Alhamisi na alisimulia jinsi alivyopata jerahan la risasi usiku wa tukio la mauaji.

Irungu alifikishwa mbele ya Jaji Grace Nzioka katika mahakama ya Milimani huku kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani ikiendelea.

Aliambia mahakama kwamba bunduki ilijifyatua yenyewe nyumbani kwa Maribe, muda mfupi baada ya kuwa na mabishano makali kuhusu baadhi ya jumbe alizoziona kwenye simu yake.

"Tulikosana tena kuhusu ujumbe niliouona kwenye simu yake na tukarushiana maneno," Irungu aliambia mahakama.

“Nilichoka nikawa natupa nguo zangu nje, nilitaka kuondoka nyumbani kwani ujumbe uleule ulikuwa unajirudia na nilikuwa nimelewa na hasira sikutaka kabisa kusikiliza, chochote nilichokuwa nimekiona,”

Anadai kuwa alipokuwa akihamisha nguo zake kutoka kwa nyumba ya Maribe na kuzitupa nje, bunduki ilitoka na kupigwa risasi kifuani.

“Kwa hiyo wakati nasogeza nguo zangu bunduki ilinitoka na kunipiga kifuani hivyo nikaenda kwa jirani yangu Brian,” aliongeza.

Mahakama pia ilisikia kuhusu jinsi alivyopata bunduki inayodaiwa kumilikiwa na jirani yake.

"Brian alikuwa ameleta bunduki kwa sababu walikuwa wakipigana na mke," alisema.

Kulingana na Irungu, aliwapa polisi maelezo yanayokinzana kuhusu jeraha lake la risasi kwa sababu mmiliki wa bunduki hiyo, Brian, alimweleza kuwa aliipata kwa njia haramu na angekuwa matatani iwapo taarifa zitatoka.

“Brian alinipa simulizi ambayo nasema majambazi walinivamia kwa sababu Brian alikuwa amepata bunduki kinyume cha sheria na akasema tukisema ukweli atakuwa matatani,” aliongeza.

Kulingana na Irungu, Maribe alifahamisha jirani yao kwamba alijipiga risasi kabla ya wote kulundikana kwenye gari la Maribe na kuelekea hospitali moja huko Langata.

"Walinipeleka hospitali ya Lang'ata lakini hawakuwa tayari kwa ajili yetu hivyo wakanipeleka hospitali ya Nairobi," Irungu alisema.

"Brian baadae alituacha nyumbani kwetu na asubuhi sikuamka mapema, mama Jackie alikuja mida ya saa tano asubuhi nikamsalimia na kurudi kulala,"

Irungu anadai zaidi kwamba aligundua alikuwa mshukiwa wa kifo cha Bi Kimani alipokuwa akitazama televisheni.

Alieleza mbele ya mahakama kuwa mwendo wa saa 6.45 asubuhi iliyofuata, maafisa wa polisi walifika mlangoni kwake na kumhoji.

“Waliomba funguo za gari, simu, kikombe na nguo niliyokuwa nimevaa wakanipeleka kituo cha polisi cha Langata wakachukua hati yangu ya kusafiria na kupelekwa kituo cha polisi Kilimani,” aliongeza.

"Nilipelekwa kwa DCI na mwanamke mmoja akanionyesha video ya CCTV akiniuliza kama ni mimi nikakataa lakini akasisitiza kuwa ni mimi, nilijifunza kwenye TV kile nilichokuwa nikituhumiwa,"

Wakati wa shauri mahakamani, Irungu alisema kuwa kaptura za cream zilizoletwa kama maonyesho hazikuwa zake. Anadai kuwa alivaa jozi ya kahawia siku hiyo.

Irungu, ambaye aliachiliwa kutoka Kamiti baada ya takriban miaka miwili kwa dhamana ya Ksh 2 milioni pesa taslimu, pia alikana kumfahamu marehemu Monica.

"Kwa kweli simfahamu Monica lakini namfahamu kaka George. Tulisoma naye 2012, hatukuwahi kuonana baada ya hapo kwa sababu nilisafiri nje ya nchi kisha tukapatana kwenye Instagram lakini tulikuwa tukutane saa arobaini na arobaini sehemu moja. Nilikuwa nikienda," Irungu aliambia mahakama.

"Sijawahi kuwasiliana naye, sikuwa na hata nambari yake,"

Jowie na Maribe walishtakiwa mwaka wa 2018 kwa mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani,amabye mwili wake ulipatikana nyumbani kwake Lamuria Gardens kaunti ya Nairobi.