Hakuna Ushahidi! Jacque Maribe aondolewa mashtaka ya mauaji

Mashtaka dhidi ya Jacque haikuwekwa ipasavyo.

Muhtasari
  • Maribe aliachiliwa huru na hakimu Grace Nzioka wa mahakama ya sheria Milimani Ijumaa juu ya ukosefu wa ushaidi.

Mwanahabari Jacque Maribe ameachiliwa huru kuhusiana na kesi ya mauaji ya  mfanyibiashara Monica Kimani.

Maribe aliachiliwa huru na hakimu Grace Nzioka wa mahakama ya Milimani Ijumaa kwa ukosefu wa ushaidi.

Alikuwa mtuhumiwa wa pili kwa kesi ya mauaji ya Monica ambayo imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya miaka 5.

Kulingana na hakimu Justice Nzioka, mashtaka dhidi ya Jacque haikuwekwa ipasavyo. 

"Ni maoni yangu kwamba shtaka lililoletwa dhidi ya mshtakiwa wa pili halikuwa shtaka sahihi" hakimu Grace Nzioka alisema.

" Je, kuna kosa nililolifanya pale mshtakiwa wa pili alipotoa maelezo kwa afisa mpelelezi wa kituo cha polisi cha Langata ambayo yalibainika kuwa si kweli? Sisemi zaidi. Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma inajua wajibu wao."