Mahakama yatoa taarifa kuhusu tukio la hakimu kupigwa risasi Makadara

Mahakama yaahidi kuimarisha usalama mahakamani baada ya hakimu kupigwa risasi Makadara.

Muhtasari

• Hakimu Monica Kivuti alipigwa risasi katika mahakama mara baada ya kutoa uamuzi katika kesi inayomhusisha mke wa afisa huyo. 

• Mokaya alisema maafisa wa polisi katika eneo la tukio walijibu na kumzuia mshukiwa.

Fridah Mokaya alipofika mbele ya JSC kwa mahojiano.
Fridah Mokaya alipofika mbele ya JSC kwa mahojiano.
Image: JSC

Msajili mkuu wa Mahakama Winfridah Mokaya ametoa taarifa kuhusu kupigwa risasi kwa hakimu na afisa che cha juu wa polisi katika Mahakama ya Makadara. 

Afisa huyo wa polisi alipigwa risasi na kuuawa siku ya Alhamisi baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi Hakimu Mkuu Monica Kivuti. Kivuti alipigwa risasi katika mahakama mara baada ya kutoa uamuzi katika kesi inayomhusisha mke wa afisa huyo. 

"Wakati wa kikao cha wazi cha mahakama mapema siku ya Alhamisi, Hakimu alifuta dhamana kwa mshtakiwa ambaye alikuwa amekiuka dhamana," Mokaya alisema. 

Alisema mshtakiwa alishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kwa kuruka dhamana. 

"Mara moja uamuzi huu ulitamkwa, afisa huyo wa polisi alimpiga risasi Hakimu na kumjeruhi kwenye nyonga," alisema. 

Mokaya alisema maafisa wa polisi katika eneo la tukio walijibu na kumzuia mshukiwa.

"..na Hakimu alikimbizwa hospitalini kwa matibabu," alisema. 

Alisema taarifa za awali zilieleza kuwa aliyempiga risasi ni askari polisi ambaye bwanake mshtakiwa. 

"Tunamtakia mwenzetu ahueni ya haraka. Pia tunatuma salamu za rambi rambi kwa familia ya afisa huyo aliyepoteza maisha katika tukio hili la kusikitisha," alisema. 

Mokaya aliwahakikishia maafisa wa Mahakama usalama baada ya kupigwa risasi kwa hakimu katika mahakama za Makadara. 

"Pia tunapenda kuwahakikishia Maafisa wa Mahakama, Watumishi na Watumiaji wa Mahakama usalama wao katika majengo yetu yote," alisema. 

Mokaya alisema wataimarisha itifaki za usalama kwa raia wanaozuru kortini pamoja na maafisa wa usalama. 

"Tunamtakia mwenzetu apone haraka. Pia tunatuma salamu za rambirambi kwa familia ya afisa huyo aliyepoteza maisha katika tukio hili la kusikitisha," alisema. 

"Tunaomba utulivu kutoka kwa watumiaji wote wa mahakama kwani vyombo vyetu vya sheria vinachunguza zaidi tukio hili."