Sisi ni binadamu pia tunahitaji usalama wetu kama madaktari-Chibanzi Mwachonda

Muhtasari
  • Katibu mkuu wa KMPDU Chibanzi alisema kwamba kuna madaktari ambao hawajapokea mishahara yao tangu mwezi wa Agosti
  • Pia alisema kwamba walituma ilani ili waanzishe mgomo wa madaktari tarehe saba Desemba, huku akisema ni ngumu lakini itabidi wagome
Chibanzi
Chibanzi

Hii leo studioni tulikuwa naye katibu mkuu wa KMPDU Chibanzi Mwachonda ambaye alizungumia mambo kadha wa kadha ambayo yanawakumba madaktari wa humu nchini.

Katibu huyo alisema kwamba bado wanaendelea kuomboleza vifo vya wenzao ambao waliaga dunia kutokana na virusi vya covid-19.

" Kumpoteza mmoja wetu ni pengo kubwa sana kwa maana utapata madaktari kumi wanawatibu wagonjwa elfu kumi, kwa hivyo tukisema tumpoteze daktari mmojakila siku ni pigo kubwa

 

Nchini kenya tuna ukosefu wa madaktari,ata sisi ni wanadamu badala ya kutia maisha yetu kwenye shida heri tukae

Tulitoa ilani na kusema kuwa mgomo utaanza tarehe saba Desemba, hatuna vifaa vya kutosha kwenye hospitali zetu

Madaktari wetu hawalipiwi bima ya afya na utapata mishahara yao imecheleweshwa na kuna wale pia hawajalipwa." Alieleza Chibanzi.

Chibanzi alisema kwamba marupurupu ambayo yalitolewa na serikali yalitolewa kwa miezi mitatu na sasa hamna kitu.

Katibu huyo pia aliweka wazi kama kila mtu ataumia ndiposa serikali ifahamu kuwa madaktari wanaumia haya basi wacha kila mtu aumie kwa maana madaktari wameumizwa sana.

Mwachonda alisema kwamba shida za madaktari zikishughulikiwa tutarudi kazini bila tatizo lolote.

Pia alisema kuwa serikali inapaswa kuweka mikakati ya kulinda maisha ya wafanyakazi wa huduma ya afya.

Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo youtube.