Nilifukuzwa shule kwa ajili ya kukuwa kwenye kikundi cha wasagaji-Mwanasosholaiti Shakilla afichua

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti Shakila aweka mambo kadha wa kadha wazi
  • Alifichua kwamba kunawakati aliwahi fukuzwa shule kwa ajili ya kujihusisha na wasaichana wasagaji

Leo studioni tulikuwa naye mwanasosholaiti Shakilla ambaye amekuwa akivuma kwa muda kwenye mitandao ya kijamii.

Shakila alifichua kwamba akiwa shule ya upili kuna wakati alifukuzwa kwa sababu alikuwa katika kikundi cha wasichana wasagaji.

"Saa hizi nina miaka 18, nakumbuka kuna wakati wazazi wangu walitwa shule baada ya mimi kupatikana nikiwa kwenye kikundi cha wasichana ambao ni wasagaji

 

nilijiunga na kikundi hicho kwa ajili rafiki yangu, tulikuwa tunakutana saa tano au nane za usiku kuzungumza maendeleo ya kikundi

Tulijulikana kisha tukatumwa nyumbani, niliwahi busu msichana mwenzake nikiwa katika kikundi hicho lakini hamna tofauti na kubusu mwanamume

Katika mtihani wangu wa kidato cha nne nilipata alama ya B+." Alieleza Shakila.

Pia alisema kwamba hakumbuki wanaume ambao amewachumbia huku akiweka wazi kwamba wanaume wangi huwa anapatana nao kupitia mitandao ya kijamii.

Shakila aliweka wazi kwamba hajawahi chumbia wanaume 97 kama ilivyosemekana awali.

Aliulizwa nini haswa huwa kinamfanya aumie roho alisema kwamba;

"Ninapoaibishwa na mashabiki kwa ajili ya mwili wangu, au watu kuniita malaya."