Nilikuwa mjumbe Ghetto radio kwa miaka 2 na nusu-Mbusi afichua

Muhtasari
  • Mtangazaji Mbusi aeleza jinsi alipata jina lake la 'Mbusi'
  • PIa alifichua jinsi aliitwa katika kampuni ya Royal Media Services lakini akakataa kuenda
Mbusi
Image: Instagram

Mtangazaji wa Radiojambo Mwangi Githinji maarufu Mbusi akiwa kwenye mahojiano alifichua mambo kadha wa kadha kuhusu maisha yake na jiinsi alikuwa mtangazaji.

Mtangazaji huyo alifichua kwamba alikuwa mjumbe kwa miaka miwili na nusu katika Ghetto redio, hii ni baada ya kutangaza trafiki kwa muda.

"Nilipoitwa Ghetto radio nilitanfaza trafiki kwa muda, baada ya hapo nilikuwa mjumbe kwa miaka miwili na nusu

Baada ya muda mfupi, nilianzisha kipindi ambapo nilipewa jina la busi hii ni baada ya aliyekuwa mpenzi wangu kuniacha

Nilikuwa nasikiza kibao cha msanii Matonya sana, kipindi chetu kilikuwa maarufu, niliitwa radiojambo nilimsihi bonoko twende naye lakini alikataa akasema Ghetto ni nyumbani hapo ndipo nilimwambia Lion twende na sasa tuko hapa

Mtangazaji Shaffi Weru ndiye alinisisitiza niende Jambo kwa maana sikuwa tayari kutoka Ghetto," Alieleza Mbusi.

PIa alifichua jinsi aliitwa katika kampuni ya Royal Media Services lakini akakataa kuenda;

"Pia niliitwa radio Citizen lakini, nilirudi kufikira jinsi napenda Ghetto, baada ya muda nilikataa ombo lao na kuendelea na kazi yangu,kila wakati namshukuru Mungu kwa ajili ya kazi yangu kwani kuna watu wengi wangeitwa MBusi lakini Mungu aliona mimi niitwe

KIla dadkika,sekunde namshukuru Mungu,"