Mwamko mpya! Radio Africa yazindua lori jipya la kunadi vituo vyake kote nchini

Muhtasari
  • Radio Africa yazindua lori jipya la kunadi vituo vyake kote nchini
Image: Victor Imboto

Kampuni ya Radio Africa Group imezindua lori jipya lililo na vifaa vya kupaza sauti na vya kisasa  litakalotumiwa na vituo vyao vya redio kuwafikia wasikilizaji mashinani.

Akizungumza na radiojambo, Mkurugenzi Mkuu , Martin Khafafa alisema kuwa vituo vya Redio Afrika ndivyo vinavyosikilizwa zaidi nchini Kenya, kampuni hiyo inataka kubadilisha nguvu hiyo na kuungana na wasikilizaji wao.

Ni ziara ambayo itafanyika katika kaunti tofauti nchini, huku safari ya ziara hiyo iking'oa nanga kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Radio Africa yazindua lori jipya la kunadi vituo vyake kote nchini
Image: Victor Imboto

Ziara hiyo imeanza na Radiojambo ambayo inafahamika kama 'One Love tour'.

 

"Ni wakati wa kusisimua kwa kampuni ni mara ya kwanza kuekeza katika lori ,kwa muda mrefu tumejulikana na wasikilizaji wetu, tunataka kuungana na wasikilizaji wetu, na tuko katika nafasi nzuri ya kuungana nao,sio jambo tu bali kila stesheni itakuwa na ziara hiyo

Tumeanza na ziara ya Radiojambo inayofahamika kama 'One love tour', baadhi ya watangazaji ambao watakuwa kwenye ziara hiyo ni pamoja na Gidi, ghost Massawe miongoni mwa wengine," Alizungumza Martin.

Aliongeza na kusema;

"Kwa mashabiki wetu tunatazamia kuwazawadi zawadi ambazo watakazoshinda wakati ziara hiyo."

Hizi hapa baadhi ya pocha za hafla hiyo;

Radio Africa yazindua lori jipya la kunadi vituo vyake kote nchini
Image: Victor Imboto
Image: Victor Imboto
Meneja mkuu Martin Khafafa akizungumza wakati wa uzinduzi wa lori jipya la kunadi vituo vyake kote nchini
Image: Victor Imboto