Orodha ya rais wa Marekani waliofanya kazi kwa muhula mmoja tu

Muhtasari
  • Orodha ya rais wa Marekani waliofanya kazi kwa muhula mmoja tu
trump.
trump.

Hivi majuzi tumeshuhudia kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha urais nchini Marekani kati ya Donald Trump na Joe Biden.

Trump alishindwa na mshindani mwenzake huku akitishia kwenda mahakamani kupinga matokeo.

Si Trump pekee ambaye alifanya kazi au kuwa rais kwa muhula mmoja bali kuna marais wengine pia walipeana mamlaka baada ya muhula wa kwanza.

 

Hii hapa orodha ya marais hao.

1.Donald Trump

Alishindwa na mpinzani mwenzake Joe Biden aliyeibuka mshindi na kuwa rais wa 46 nchini humo.

2.George.H.W. Bush

Alikuwa rais wa marekani mnamo mwaka wa 1989 hadi mwaka wa 1993, ambapo alikuwa rais wa 41 nchini humo.

George alikuwa rais kwa muhula mmoja tu.

3.Herbert Hoover

 
 

Ndiye alikuwa rais wa 31 Marekani huku akiwa mamlakani kutoka mwaka wa 1929 hadi mwaka wa 1933 na ambaye alikuwa rais kwa muhula mmoja.

4.Jimmy Carter

Alikuwa rais wa 39  nchini Marekani huku akiwa rais kutoka mwaka wa 1977-1981.

5.Gerald Ford

Alikuwa rais kwa muhula mmoja na kuwa mamlakani tangia mwaka wa 1974-1977.

Miongoni mwa marais wa Marekani waliokuwa rais kwa muhula mmoja ni pamoja na William Howard Taft,Grover Cleveland miongoni mwa wengine.