Mambo ambayo mwanamke hatawahi mfanyia mwanamume kama anampenda

Muhtasari
  • Mambo,5, ambayo mwanake hawezi kuyafanya kama anampenda mwanamume

Kuwa katika uhusiano wa kimapenzi wakati huu ni ngumu sana kwa wanawake wengi iwapo hutampa pesa endapo anazihitaji.

Kuna wale ambao wataelewa kuwa huna pesa, na kuwa unajaribu uwezavyo kumpenda na kutimiza mahitaji yake lakini kuna wale kamwe hawataelewa hali yako ya maisha.

Kama mwanamke anakupenda kama asemavyo haya basi kuna mambo ambayo hatamfanyia mwanamume.

 

Mambo hayo ni kama vile yafuatavyo;

1.Kukutumia

Wanawake wengi wa karne hii ya sasa watatumia mwanamume na kisha wamteme na kusahau kama walikuwa pamoja baada ya kukutumia na kukufilisisha.

2.Kutokuheshimu

Kama mwanamke kwa kweli anasema anakupenda hata ufanye nini atadumisha heshima yake kwake na wala hatoweza kutupilia heshima hiyo mbali.

Haya basi kama mwanamume ukimuona mke wako hakuheshimu basi mteme kwa maana hata ukimuoa hatawahi kukupa heshima kama mwanamume wa nyumba.

3.Kutumia pesa zako vibaya

 

Mwanamke mwenye akili zake atatumia pesa ya mwanamume vizuri na hatoweza kutumia kwa nunua bidhaa ambazo hazistahili, kama ameanza tabia kama hiyo ndugu yangu funga kiatu mshipi jipe shughuli.

4.Kukudanganya

Kama kwa kweli mwanake anakupenda hatakudanganya na mwanamume yeyote yule bali ata kuwa mwaminifu kwako na kuvumilia mambo yote na wala hatakuwa na tamaa ya kutaka mwanamume mwingine.

5.Kutokuwa salama

Mwanamke kama anakuelewa na kukuamini huwa anafurahi na kuwa na utulivu endapo una marafiki zako ata kama ni wanawake.

Bali ukimpa sababu ya kutokuwa salama haya basi hutakuwa na amani