Shida ni nini?Sababu ambazo walimu wengi wanastaafu wakiwa maskini

Muhtasari
  • Sababu ambazo zinachangia walimu wengi kustaafu wangali maskini
TSC
TSC

Tumeshuhudia walimu wengi wakiteseka haswa wakati huu wa janga la corona, wengi walianza vibarua na hata kuanza kiguu na niia ili kutafuta riziki ya kila siku.

Kwa kawaida walimu wengi hupata mshahara kila mwisho wa mwezi kama uchumi umeenda vyema nchini.

Lakini kuna tatizo moja ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza kila kuchao na kila dakika, kwanini walimu wengi baada ya kustaafu ni maskini?

Licha ya wao kupokea pesa wengi hurudi nyumbani mikono mitupu, ilhali wahenga walisema kwamba mkono mtupu haulambwi.

Haya basi husitie shaka hizi hapa sababu kwanini walimu wengi wakistaafu ni maskini kupindukia;

1.Tamaa

Wengi wao hupatwa na tamaa wakati wameeona kitu fulani sokoni, ana ahidi moyo wake ya kwamba lazima apate kitu hicho endapo atapata mshahara.

Baada ya kupata mshahara wao wanaaribu pesa kwa mambo yasiyostahili.

2.Kujihusisha na uraibu

Naadhi ya walimu wakipokea mashara wao hawawekezi chochote bali huwa wanaenda kulewa pesa zao na kesho unapomuomba shillingi kumi hana chochote hata pesa ya chakula.

 

3.Kuchukua mikopo ili kuendeleza mtindo wa maisha 

Kwa kawaida wengi wanataka kutembea na magari ya kifahari ndio utanunua gari hilo bali kila siku litakuwa linahitaji mafuta.

4.Kukosa mpangilio wa jinsi wa kutumia pesa zake za kustaafu

Baada ya kufanya kazi kwa miaka yote si wote ambao watawekeza au kuwa na mpanfo wa jinsi wa kutumia pesa za ustaafu naa vile atasaidia familia yake.

Ni jambo lipi walimu wanapaswa kuzingatia endapo wamestaafu?