Orodha ya magavana ambao walikuwa walimu kabla ya kujiunga na siasa

Muhtasari
  • Orodha ya magavana ambao walikuwa walimu kabla ya kujiunga na siasa
Okoth obado
Gavana wa Migori Okoth Obado Okoth obado

Lazima kila mwananchi awe na mwanzo mdogo kwa maana ni hali ya maisha , lakini kuna wale walianza na mwanzo mdogo na mwishowe kuwa watu mashuhuri nchini.

Leo katika makala haya tunaangazia magavana ambao walikuwa walimu wa shule mbalimbali kabla ya kujiunga na siasa.

Hii hapa orodha ya magavana wa nchi ya Kenya ambao walikuwa walimu kabla ya kuwa katika sekta ya siasa.

 

1.Gavana James Ongwae

ongwae alikuwa mwalimu ambaye alifundisha katika shule kadhaa kabla ya kujiunga na siasa za humu nchini.

Ongwae ni gavana mteuliwa katika kaunti ya Kisii.

2.Sospeter Odeke Ojaamong

Ni gavana wa kaunti ya Busia na ambaye alikuwa ni mwalimu wa Biolojia na Kemia.

3.Okoth Obado

Licha ya kuwa na kashfa nyingi na kukamamtwa na kisha kujibu mashtaka gavana wa Migori Obado alikuwa pia mwalimu.

 

4.John Obiero Nyagarama

Yuko katika muhula wa pili katika kazi yake ugavana, Obiero ni gavana wa kaunti ya Nyamira, katika makala au orodha hii hakuachwa nyuma kwa maana pia alikuwa mwalimu.