Sema kuachwa mtaani

Aliniacha na kutokomea kama jini,bila kwaheri au sababu

Sonia anasema ingekuwa bora kuambia sababu yake kwenda

Muhtasari

 

  •  Wanawake wengi huwa waatthiriwa wa tukio la kuacha bila neno lolote kusema 
  •  Sonia anasema angependa tu kujua tatizo lilikuwa nini 
  • Wakati mwingine ni bora kuendelea na maisha yako bila kujisumbua kutafuta sababu ya kukwepa kwa mtu  maishani mwako 

 

  Sonia Nyaboke  hapati usingizi kila siku kwa sababu ya masaibu yaliompata tangu   mwanamme waliyekuwa wameanza naye uhusiano kukatiza mawasiliano ghafla na kuingia mitini . Sonia anasema tatizo ni kwamba hana machungu kwamba aliachwa , makovu yake hasa ni kwa ajili ya namna alivyoachwa kwa sababu ni bora iwapo mtu hakupendi au ameabadilishania kuhusu uhusiano weni akueleze   ujue ni kwa nini uhusiano wenu haukudumu 

 Alivyoachwa kighafla hivyo ni hatua ambayo imempa maswali mengi kuliko anavyoweza kujibu kwa sababu hafahamu iwapo kuna kitu au jambo ambalo Eric alona kwake na kuamua kukwepa ama  alikuwa tu na nia ya kuridhisha hamu zake za kimwili na kisha kusonga mbele . Anajutia kwa sababu muda huo wote wa miezi sita ,alimpa moyo wake wote na hata mipango ilikuwa ishaanza kufikiria ya maisha yao pamoja katika siku za usoni .Hawakugombana wala hapakuwa na lolote la kumfanya atoroke bila kusema lolote ni hicho ni kiini kikubwa cha machungu yake Sonia .

  Hatua hiyo ,ya kuachwa hoi na mwanamme  baada ya kumfunguliwa moyo wake wote imemtia woga Sonia  kuhusu masuala ya mahusiano na anahofu huenda woga huo wake ukawafungia nje ya maisha yake wanaume ambao labda wana nia njema ya kumpenda kiukweli .

  Mchakato mzima wa kuacha hoi ulianz wakati Eric alipoanza kujibu jumbe zake ni kana kwamba hataki . Ikawa kila mawasiliano yao yalikuwa yakileta jibu la neon moja kama vile ‘sawa’,’okay’, ‘Yes’, ‘No’, Alright’, ‘Good’ na kadhalika . Kisha  kikafuatia kipindi cha  siku tatu bila mazungumzo kato yao. Eric alikuwa mtu wa kutuma tuma jumbe za kumjulia hali kila wakati . Soni alianza kushtuka wakat siku mbili nzima zilipokwisha bila ujumbe wowote kutoka kwake na hata hakuwa ajibu jumbe zake . Ikawa siku mbili zikaongezeka kuwa  wiki moja kisha ya pili hadi miezi miwili sasa imekwisha na akiangalia mtandaoni jumbe anazomtumia zinamfikia  na anazisoma ila hajibu .

  Uhusiano wake huo ulikwisha bila mtu kusema lolote . Soia anashangaa iwapo ni yeye pekee amekuwa mwathiriwa wa mwanamme kumuacha bila sababu wala kusema lolote na  ni ipi sababu ya mtu kukuacha kwa njia kama hiyo .