Kizungumkuti

Baby daddy anavuruga maisha yangu ya mapenzi-siwezi kuwa na uhusiano!

Stella anasema anataka kupiga hatua mbele na maisha yake

Muhtasari

 

  •  Stella amejaribu karibu mara tatu akiwa katika mahusiano na mwanamme mwingine ,Baby Daddy huyo hufanya kila awezalo kuvuruga mahusiano hayo
  • Stella anasema hilo halikufaulu kwani baada ya muda wa wiki chache alimrudisha mtoto akisema  imekuwa vigumu kumlea mtoto na pia kufanya kazi yake .

 

sad woman
sad woman

Wakati mnapoachana na mwanamme ambaye alikupa uja uzito na kisha akakosa kukuoa ,maisha huchukua mkondo mwingine na wakati mwingine ni bora kila mtu achukue mkondo wake wa maisha ila tu inapolazimu kwamba mzungumze kwa sababu ya mtoto aliyetokana na uhusiano wenu .

Kwa wengine hilo huwa rahisi kwa sababu ni wengi ambao walizaa watoto na wanaume wengine ambao hufahamika kama baby daddy kisha wakajipata katika ndoa na  mtu mwingine na maisha kuendelea bila bughdha zozote. Lakini hali sio rahisi kwa Stella , kwa sababu mwanamme ambaye alimvunja ubikira na kumpa mimba hadi leo amekataa kabisa kumpa nafasi ya kuendelea na maisha yake hasa  katika mahusiano ya aina yoyote licha ya kwamba waliachana na kinachowaunganishani mtoto . Lakini mwanamme aliyempa mimba  na kisha kumuacha hajampa Stella nafasi ya kuendelea na maisha yake hasa  ya kupata mtu mwingine na kuishi kama watu wengine . Kila anapopata fununu kwamba Stella ameanza uhusiano na mwanamme mwingine yeye huanza tena  kujipendekeza kwa Stella akisema anataka warudiane waishi kama mke na mume . Baadaye atafanya kila awezalo kumtimua mwanamme yeyote anayejaribu kumjua Stella akisema kwamba Stella ni mke wake licha ya kwamba awali hakuwahi kumtambua kama mke wake .

  Stella amejaribu karibu mara tatu akiwa katika mahusiano na mwanamme mwingine ,Baby Daddy huyo hufanya kila awezalo kuvuruga mahusiano hayo . Anasema imekuwa vigumu kwake kupiga hatua mbele na maisha yake kwa ajili ya kushikwa na minyororo ya mwanamme huyo  waliyezaa naye mtoto na wakati mwingi anatumia kisingizio cha kutaja kuja kumuona mtoto wake ili kumchunguza Stella na kujua kinachofanyika katika maisha yake ya kibinafsi.

  Stella anasema wakati moja babu daddy huyo alimpata na mpenzi wake wa wakati huo chumbani mwake na akazua vita huku mtaa mzima ukishangaa ,watu wakifikiri kwamba yeye kama mke wa mtu alikuwa amefanya kibaya kwa kumleta mwanamme mwingine katika nyumba yake . Tangia hapo Stella alisimama kidete kumtaka  baby daddy aondoke kabisa katika maisha yake ya ndani na hata akawa tayari kumkabidhi mtoto wao ambaye alikuwa na umri wa miaka sita wakati huo ili asiwe na kijisababu cha kutaka kuja kwake . Stella anasema hilo halikufaulu kwani baada ya muda wa wiki chache alimrudisha mtoto akisema  imekuwa vigumu kumlea mtoto na pia kufanya kazi yake .