Nguvu za kiume

Patikana! Jinsi tembe za kusisimua nguvu za kiume zilivyovunja ndoa yangu

Tembe ya kuongeza nguvu za kiume yavuruga ndoa ya Eliud

Muhtasari

 

  • Anasema mkewe alikuwa tayari kumsamehe iwapo angepata hata mpira ya  kondomu lakini tembe ya kusisimua nguvu za kiume ni kitu ambacho hakufikiri mume wake angejihami nacho ili kuwafurahisha na kuwaridhisha wanawake wa pembeni
  • Haelewi jinsi alivyosahau kuitoa mfukoni pakiti hiyo iliyokuwa na tembe hizo  na mkewe alivyozipata ,hakuendelea na shughuli za kuosha nguo kwani aliutoa ushahidi huo na kumgonja arejee nyumbani

 

Eliud  Musyoki   yupo katika majuto kwa sababu  tabia zake zimemfanya  kuacha na mkewe ambaye alipata tembe ya kusisimua nguvu za kiume katika mfuko wa nguo yake akiosha nguo .

 Ni kitendo ambacho hadi leo kinampa  huzuni sana kwani hakuwa njia nyingine ya kujitetea kwani kulingana naye , hakuwa akiitumia tembe hizo wakati wa kushiriki mapenzi na mkwe lakini huko nje ya ndoa alikuwa na msururu wa wanawake aliokuwa akila uroda   nao na alihitaji usaidizi wa nguvu za tembe hizo kufanya maangamizi yake . Anasema mkewe alikuwa tayari kumsamehe iwapo angepata hata mpira ya  kondomu lakini tembe ya kusisimua nguvu za kiume ni kitu ambacho hakufikiri mume wake angejihami nacho ili kuwafurahisha na kuwaridhisha wanawake wa pembeni

 Eliud anasema kupatikana kwake kulijiri wakati ambapo alikuwa mwenyewe ashaamua kuacha tabia za kwenda nje ya ndoa na tayari alikuwa  ameshakatiza mahusiano yake na wanawake karibu wawili waliokuwa  wakijatambua kama wapenzi wake wa pembeni .

Haelewi jinsi alivyosahau kuitoa mfukoni pakiti hiyo iliyokuwa na tembe hizo  na mkewe alivyozipata ,hakuendelea na shughuli za kuosha nguo kwani aliutoa ushahidi huo na kumgonja arejee nyumbani .  Eliud anasema hakupata hata nafasi ya kusema lolote kwani cha kwanza alichopepezewa usoni akitakiwa kueleza anafanya  nazo ni tembe hizo na hapo ndipo alipojua maisha yake ya ndoa yalikuwa  yamefika mwisho

  Juhudi zake kujaribu kumdanganya mkewe kwamba tembe hizo sio zake ziliambulia patupu kwa sababu tayari alikuwa ashaitumia tembe moja iliyokosekana katika pakiti hiyo na usiku uliotangulia hakuwa amelala nyumbani akitoa kisingizo cha kufanya kazi usiku  wote .  Mkewe hakuhiaji kuwa mwanasayansi kugundua kwamba usiku huo ndio ambao Eliud alikuwa ameitumia tembe hiyo moja ambayo haikuwepo katika pakiti ile .

   Akifikiri mkewe angeacha ugomvi kisha maisha yaendelee kama kawaida kwani wameshangombana mara nyingi katika ndoa yao ,Eliud alishangaa kumuona mama ya watoto wake akifunga virago na  kila chake pamoja na watoto wao watatu na kuondoka asionekane tena ama kutaka hata kuzungumza  na Eliud.Hivyo ndivyo tembe ya kusisimua nguvu za kiume ilivyovunja ndoa ya Eliud miaka minne iliyopita