Mapenzi ya Hospitalini

Unaanzaje? Nilivyopendana na daktari wangu nikiwa hospitalini

Mgonjwa na daktari wake wapendana hospitalini

Muhtasari

 

  • Joyce alikuwa amelazwa hospitalini kwa muda wa miezi mwili baada ya kugongwa na gari na kisha dereva wa gari hilo kutoroka bila kusimma ili kumsaidia
  • Muiru anasema  kuzungumza mara kwa mara na Joyce kulimfanya atambue umuhimu  wa mtu kuwa na Imani kwa mungu na siku baada ya nyingine mvuto huo ulizidi kuongezeka na uhusiano kati yao ukaboreka hata Zaidi baada ya Joyce kuruhusiwa kwenda nyumbani .
  •  Joyce anasema kukutana na Muiru katika mazingira yale ya  hospitali ni  dhihirisho kwamba mapezni hayachagui yatakupata wapi kwani hata hospitalini ambako labda mtu atafikiri kuna huzuni mwingi na woga ,watu wanaweza kukutana na kukupendana

 

Joyce  Khavetsa* akisimulia jinsi alivyokutana na mpenzi wake daktari David Muiru utafikiri ni simulizi kutoka kwa filamu ama kitabu cha mwigo lakini ndio kisa halisi cha jinsi walivyokutana na  mapenzi yao kunawiri .

Joyce alikuwa amelazwa hospitalini kwa muda wa miezi mwili baada ya kugongwa na gari na kisha dereva wa gari hilo kutoroka bila kusimma ili kumsaidia .Alikimbizwa katika hospitali moja ya kibinafsi huko Embu na Muiru ndiye aliyekuwa daktari  wa kwanza wa dharura kumhudumia . Anasema baada ya  wiki kadhaa alianza kupata nafuu na kutembea tembea nje ya hospitali hiyo alikolazwa na mara nyingi ni daktari Muiru ndiye aliyekuwa akija kumjulia hali na kisha kutoa maagizo kwa wauguzi kumkokota nje  ili aote jua ama atembee tembee kunyoosha viungo vya mwili wake .

  Joyce anasema alivutiwa sana na utunzi wa Muiru ambaye alionekana kumjali wakati alipokuwa akimtibu na kumfuatilia kila siku ili kuhakikisha kwamba hali yake inaboreka .Alipoondoka hospitalini ,alianza kujipata akimfikiria sana daktari aliyemtunza akiwa hospitalini .  Muiru naye alikuwa akiendelea kumpigia simu  Joyce hata alipoondoka hopsitalini na hata kumzuru nyumbani kutazama jinsi alivyokuwa akiendelea kuboreka .

Muiru anasema yeye kilichomvutia sana kwa Joyce ni ujasiri wake wa kutaka kuishi kwani alivyopata ajali ile ,aliachwa katika hali mbaya lakini akipewa matibabu alikuwa akionyesha matumaini makubwa ana ya kutaka kuishi na alipigania  hali yake kando na kwamba pia alikuwa mcha mungu sana .

   Muiru anasema  kuzungumza mara kwa mara na Joyce kulimfanya atambue umuhimu  wa mtu kuwa na Imani kwa mungu na siku baada ya nyingine mvuto huo ulizidi kuongezeka na uhusiano kati yao ukaboreka hata Zaidi baada ya Joyce kuruhusiwa kwenda nyumbani . Madaktari wengi waliokuwa wakifanya kazi na Muiru hushangaa sana jinsi wawili hao walivypendana na hata wao humfanyia Muiru utani kwamba ‘alipenda mgonjwa wake’ . Joyce anasema uhusiano wao wa kimapenzi ulianza kikamilifu wakati alipoondoka hospitalini na wakati mwingi wangekutana na Muiru na kuzungumza kwa muda mrefu kuhusu masuala mbali mbali .

Anasema wengi hawakuamini alipowafichulia kwamba ameanza kupendana na daktari wake ambaye alikuwa mtua wa kwanza kumhudumia wakati alipofikishwa hospitalini wakati alipogongwa na kuachwa hoi barabarani .

 Joyce anasema kukutana na Muiru katika mazingira yale ya  hospitali ni  dhihirisho kwamba mapezni hayachagui yatakupata wapi kwani hata hospitalini ambako labda mtu atafikiri kuna huzuni mwingi na woga ,watu wanaweza kukutana na kukupendana