- Mama’s boy hufuata kila wanachoambiwa na mama yao na wakati mwingi hilo huvuruga uhusiano wao na wapenzi wao au hata rafiki zao.
- Kila mtu ana udhaifu wake lakini kwa mama’s boy –mamake ni malaika, anayajua yote na hawezi katu kukosolewa.
Umeyaskia mengi kuhusu msemo huo wa wanaume ambao kila linalosemwa na mama yao ni sheria na hivyo basi kauli za mama zao hutawala maisha yao kuanzia kila uamuzi wanaofanya.
Imekuwa vigumu kwa wanawake wengi kuwa katika uhusiano wa kudumu na wanaume ambao huitwa mama’s boy kwa sababu wakati wote lazima kivuli cha mama yao kiwe nyuma yako. Kama Diamond Platinumz wa Bongo, imefahamika kwamba mahusiano yake na msururu wa wanawake wote hao umekuwa ukivurugwa na muingilio wa mamake Sandra Dangote
Mama’s boy hufuata kila wanachoambiwa na mama yao na wakati mwingi hilo huvuruga uhusiano wao na wapenzi wao au hata rafiki zao. Sasa hizi hapa baadhi ya ishara za kujua kwamba mwanamme ambaye upo katika mahusiano naye ni mama’s boy na wakati wote itakuwa ni ushindani kati yako na mamake.
Mtu wa kwanza kumkimbilia ni mamake
Akiwa na tatizo hivi basi mtu wa kwanza kujua ni mamake. Iwapo ana habari njema za kusema basi fahamu kwamba mamake ndiye atakayekuwa wa kwanza kujuzwa hata akiwa na mke, anachosema mamake ni sheria, anachopinga mamake basi ni mwiko
Wanapenda kuishi na mama yao
Kuna sababu nyingi za mtu mzima anayejiweza kutaka kuishi na mamake kwa mfano iwapo mama ni mgonjwa au wataka kuokoa fedha kwa kuepuka kulipa kodi lakini mama’s boy ataishi na mamake hata iwapo ana miaka 40 na zaidi. Wakati mwingi hana haraka ya kuhamia kwake na isitoshe mamake ndiye humfulia nguo.
Huwezi kumkosoa mamake
Kila mtu ana udhaifu wake lakini kwa mama’s boy –mamake ni malaika, anayajua yote na hawezi katu kukosolewa. Ukitilia doa mamake basi wewe utakuwa adui mkubwa. Hata iwapo mamake ana kosa na ni la wazi, utafanya kosa kubwa sana kwa mama’s boy kumkosoa mamake.
Mama ndiye jaji mkuu
Maamuzi muhimu ya kibinafsi hata yanayomhusisha mkewe yatafanywa na mama mtu. Ataamua wajukuu wake wataenda shule gani, mtajenga nyumba aina gani, shamba mtanunua wapi na hata siku ya krisimasi mtapika nini …Ataamua hata wakati wa kumpata mtoto mwingine au ni njia gani ya kupanga uzazi unayofaa kutumia ..
Kuishi katika boma moja na mama mkwe ambaye uhusiano wake na mwanawe ni wa chanda na pete ni kama kuishi jela kwa baadhi ya wanawake. Huna uhuru .
Kwa mfano, wakati Diamond alipokuwa pamoja na Tanasha, Mama Dangote alikuwa akidhibiti kila hali ya maisha yao. Tanasha amesema wakati mwingine aliamua kujituliza kama mkaza mwana mwema kwa kunyamza lakini hilo kwa kweli halikumsaidia.
Zari naye pia alizingumza tabia hiyo ya mama Dangote kuingilia kabisa maisha ya kibinafsi ya Diamond lakini wengi walifikiri kwamba labda Zari alikuwa na machungu baada ya kutengana na msanii huyo.
Iwapo bado wataka au upo katika uhusiano na mama’s boy basi jitayarishe kwa msururu wa kesi ambazo utashindwa wakati mwingi.