- Jared Akitoto alikuwa amejiundia pesa kwa muda mrefu na sio kupitia kazi yake ya ualimu bali kuwauzia wanafunzi wake bangi kutoka nchi jirani ya Uganda .
- Chini ya uchapoakazi wake na upole ambao mwalimu Jared alikuwa nao,kulikuwa na siri kubwa ambayo ni wanafunzi watundu waliokuwa wakitumia dawa za kulevya ndio waliofahamu .
Shule moja ya upili huko Malaba miaka kadhaa iliyopita ilijipata katika vyombo vya habari kwa sababu zisizokuwa nzuri .Hii ni baada ya kulipuka kwa kava ya mwalimu mmoja aliyekuwa ameandikwa kazi na bodi ya usimamizi wa shule aliyekuwa akiwauzuia wanafunzi mihadarati na hasa bangi.
Jared Akitoto alikuwa amejiundia pesa kwa muda mrefu na sio kupitia kazi yake ya ualimu bali kuwauzia wanafunzi wake bangi kutoka nchi jirani ya Uganda . Alikuwa ameweka mikakati kabambe ya kuzuia kugunduliwa na waliokuwa wakimjua baadaye hawakuamini alipokamatwa kwa hatia hiyo kwani licha ya mkuwa mwalimu chapa kazi ,alikuwa pia amejituma kuwasaidia wanafunzi wake kwa mafunzo ya mambo kama michezo na hata aliiongoza timuya shule hiyo katika mashindano ya kanda na wakafika kiwango cha mikoa . Chini ya uchapoakazi wake na upole ambao mwalimu Jared alikuwa nao,kulikuwa na siri kubwa ambayo ni wanafunzi watundu waliokuwa wakitumia dawa za kulevya ndio waliofahamu . Jared alikuwa ameunda mtandao wa ushirikiano shuleni humo ambapo angezileta dawa za kuleya zilizohifadhiwa shuleni .Miongoni mwa waliomsadia kuziuza dawa hizo ni wapishi wa shule na hata wafanyikazi waliokuwa wakiingia na kutoka mle shuleni .
Shehena kubwa ya bangi ingeletwa kutoka Uganda hadi kwake ,kisha aangeipakia katika misokoto na kisha kuipeleka shuleni ambapo wapishi wangemsaidia kuificha .baadaye bangi hiyo ingeuzwa kwa wanafunzi wakati wa usiku na hata wakati wa shughuli za michezo au safari za nje ya shule ,kungekuwa na wakala wake miongoni mwa wanafunzi ambaye angeendelea kuziuza dawa za kulevya kwa wanafunzi wa shule jirani na hata watu wa nje .
Palipotokea ripoti kwamba wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wakitumia bangi na visa vya utovu wa nidhamu kuongezeka ,mwalimu mkuu alishangaa wanafunzi wake walikuwa wakitoa wapi bangi . Uchunguzi wa kisiri ulianzishwa na shule na hata kuwahusisha polisi . Wakati wapishi wawili walipokamatwa wakiwa na misokoto ya bangi ,siku ya 40 kwa mwalimu Jared ilikuwa imekaribiwa.walihojiwa na kutakiwa kusema wote waliohusika na biashara ya mihadaratai shuleni . Walipomtambua mwalimu Jared kama kiongozi wa mtandao wa uuzaji wa mihadarati ,kila mmoja shuleni humo aliachwa kinywa wazi .
Hakuna aliyeamini kwamba mwalimu huyo mpole na chapakazi alikuwa na ukatili wa kuwauzia wanafunzi wake dawa za kulevya akijua fika madhara yake. Jared alikamatwa na polisi walipomfikisha kwake ,shehena ya dawa za kulevya walizopata iliwashangaza. Mwalimu Jared alishtakiwa na kufungwa jela ,tamaa yake ya kutengeza pesa kwa kuhatarisha maisha ya wanafunzi ikaishia kumuacha bila kazi ya ualimu na majuto chungu nzima .